Home » » MAKAMU WA PILI AKUTANA NA KAMATI YA MAADILI YA BUNGE

MAKAMU WA PILI AKUTANA NA KAMATI YA MAADILI YA BUNGE

Written By CCMdijitali on Wednesday, February 23, 2022 | February 23, 2022

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokutana nayo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiziungumza na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokutana nayo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.

 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuwia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) ACP Ahmed Khamis Makarani akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar juu ya ujio wa Taasisi mbili za kuzuwia rushwa nchini Tanzania ofisini kwake vuga Jijini Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza kamati ya Haki,maadili na madaraka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kusimamia misingi ya kisheria na haki za wabunge.

Mhe. Hemed ametoa Pongezi hizo alipofanya mazungumzo na Kamati hiyo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.

Amesema Kamati hiyo ni muhimu sana kwa Bunge ambapo kwa misingi ya Sheria iliyopo inawajibika vyema kwa kuweza  kusimamia nidhamu ndani na nje Bunge na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa na wabunge hao katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

Mhe. Hemed amesema Kamati hiyo inasimamia misingi ya maadili kwa kuhakikisha Bunge linajengeka kwa kufata maadili na uwajibikaji kwa viongozi hao na kusema  kuwa muhimili wa Bunge upo Imara kwa maslahi ya Watanzania wote.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wajumbe wa kamati hiyo kuendelea kulitumikia Bunge kwa kuwajibika na kuongeza mashirikiano baina yao jambo ambalo litaongeza uwajibikaji katika majukumu yao ya kila siku.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameipongeza kamati hiyo kwa kuamua kukutana na kamati ya maadili na kinga za wajumbe ya baraza la wawakilishi la Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu,na kusisitiza mashirikiano baina yao ili kuzidi kubadilishana mawazo ya kuendesha na kusimamia kamati hizo.

Mhe. Hemed ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kuijenga Tanzania yenye maendeleo na kuwataka viongozi wa kamati hizo kuwasaidia viongozi hao katika kuiletea Tanzania maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Haki maadili na madaraka ya bunge Mhe EMMANUEL A. MWAKASAKA ameshukuru Bunge kwa kuwaaamini kuwateuwa katika Kamati hiyo na kuahidi kusimamia vyema majukumu  yao kwa ueledi ili kujenga nidhamu ndani ya Bunge kwa maslahi ya Tanzania.

Pia mhe MWAKASAKA amemshukuru Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Tulia Akson kwa kuisimamia Kamati hiyo katika kuendesha majukumu yao ikiwemo kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara jambo ambalo linawaongezea uzoefu katika majukumu yao ya kila siku.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya maadili na kinga za wajumbe ya Baraza la Wawakilishi Mhe. PANYA ALI ABDALLA amesema kuwa Baraza limefarijika kwa ujio wa Kamati hiyo hatua ambayo imetoa fursa ya kuwakutanisha wajumbe wa Kamati hizo za Mihimili  miwili kuweza kubadilishana mawazo na kumuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa wataendeleza mashirikiano hayo kwa kuongeza nidhamu ndani ya Muhimili mitukufu ya kutunga na kubadilisha sheria.

 

……………………………….

Abdulrahim Khamis

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

23 /02/2022

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link