Home » » WATUMISHI WATANO WASIMAMISHWA KAZI MASASI MJINI

WATUMISHI WATANO WASIMAMISHWA KAZI MASASI MJINI

Written By CCMdijitali on Wednesday, February 9, 2022 | February 09, 2022

 




Watumishi Watano wa halmashauri ya Mji Masasi Mkoani Mtwara, wamesimamishwa kazi akiwamo mweka hazina na mkuu wa idara ya mipango, huku wengine Wawili wakipewa onyo kutokana na kukabiliwa na tuhuma mbalimbali za ukiukwaji wa sheria za serikali zikiwamo sheria za fedha na Manunuzi.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Elias Ntirihungwa, amesema hatua hiyo imekuja baada ya watumishi hao kuwa miongoni mwa watumishi 14 waliotajwa katika ripoti ya ukaguzi maalumu uliofanyika kati ya Mwezi Mei na Julai mwaka 2021.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link