Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa |
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa leo Februari 24, 2022 anatarajia kumuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa kumi wa wakuu wa nchi wa Serikali zinazohusika na
mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano nchini DRC na kwenye ukanda wa
maziwa makuu unaofanyika, jijini Kinshasa, DRC
Mkutano wa Kumi wa
Wakuu wa Nchi na Serikali unatarajia kupitisha Taarifa va Pili
Utekelezaji wa Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano kwenye Ukanda wa
Maziwa Makuu na kupitisha Maazimio ya Mkutano huo
Mkutano wa
Wakuu wa Nchi na Serikali unatarajiwa kuongozwa na Mhe. Félix Antoine
Tshisekedi Tshilombo, Rais wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) baada
ya kukabidhiwa Uenyekiti na Mwenyekiti wa sasa Mhe. Yoweri Kaguta
Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda.