Home » » ZIARA YA MKUU WA WILAYA KASKAZINI B HOSIPITALI YA PANGATUPU - ZANZIBAR

ZIARA YA MKUU WA WILAYA KASKAZINI B HOSIPITALI YA PANGATUPU - ZANZIBAR

Written By CCMdijitali on Thursday, February 10, 2022 | February 10, 2022

 

Wilaya ya kaskazini B


Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Hamid Seif Said hajaridhishwa na hali ya Ujenzi wa hospital ya Wilaya Pangatupu na kuagiza kampuni ya World Class Engineering Contract kuongeza bidii ili waweze kuendana na muda waliokubaliana na serikali

Akizungumza na watendaji wa kampuni  hiyo wakati alipofanya ziara ya kutembelea mradi huo Amesema Kasi ya Ujenzi ni ndogo hivyo ni vyema kampuni hiyo ikabainisha matatizo yanayosababisha kuzorota Kwa shughuli za Ujenzi Ili yaweze kutafutiwa ufumbuzi wa haraka

Amesema serikali ya wilaya ipo tayari kushirikiana na kampuni hiyo wakati wote wa Ujenzi Ili kuhakikisha hospital inayojengwa inakamilika Kwa wakati na Kwa kiwango kinachotakiwa

Amesema serikali imeamua kuipa mradi kampuni hiyo kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wao hivyo ni vyema Kwa kampuni hiyo kuonesha uwezo wao Kwa serikali

Amesema ni miezi miwili tangu kuanza Kwa Ujenzi wa hospital hiyo lakini ni jambo la kushangaza kuona Ujenzi huo ukiwa katika hatua za awali wakati mkataba wa Ujenzi unakamilika mwezi June mwaka huu

Akizungumzia kuhusu tatizo la kampuni hiyo kuchukua wafanyakazi kutoka nje ya wilaya hiyo Hamid Amesema kitendo hicho sio kizuri kwani serikali imekuwa ikiagiza kutoa kipaumbele cha ajira Kwa wananchi wazawa katika miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuinua kipato Cha wananchi wake

Msimamizi wa mradi kutoka kampuni ya world class engineering contract bwana Mgwasa Godfrey Takao Amesema kuzorota Kwa mradi pamoja na kuchelewa kwa malipo ya wafanyakazi  kunatokana na kucheleweshwa Kwa fedha kutoka serikalini 

Hata hivyo Amesema kampuni hiyo inakusudia kufanya kazi usiku na mchana  pamoja na kuongeza wafanyakazi wengine Ili kumaliza Ujenzi wa hospital hiyo kwa wakati

Mapema wakiwasilisha malalamiko yao Kwa mkuu wa wilaya baadhi ya wafanyakazi wamesema wamekuwa wakifanya kazi Kwa muda mrefu pamoja na kucheleweshewa  fedha zao ambapo hadi Sasa wamefanya kazi wiki mbili bila ya malipo yoyote  Hali ambayo inawapa usumbufu wa kutoa  huduma Kwa  familia zao.

Ujenzi wa hospital ya Wilaya pangatupu ni miongoni mwa hospital 10 zinazojengwa na serikali kupitia mradi wa fedha za COVID 19 na unatarajiwa kujengwa Kwa kipindi Cha miezi sita kuanzia January mwaka huu
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link