BASHUNGWA AWATAKA WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA KUPANGA MACHINGA DODOMA.
Na Angel Msimbira TAMISEMI
Wito huo umetolewa Leo tarehe 12 Machi, 2022 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa wakati wa ziara yake na wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala, na Wakurugenzi wa mikoa yenye hadhi ya majiji kutembelea ujenzi wa eneo hilo.
Akizungumza na viongozi hao, Bashungwa alisema Rais Samia Suluhu Hassan ametambua sekta ya machinga kuwa rasmi hivyo kwa sasa wanaenda na maono yake ya kuhakikisha wanajengewa mazingira rafiki kwa kazi zao.
Amesema kuwa ingewezekana kwenda nje ya nchi kubuni kitu ambacho tunaweza kujifunza sisi wenyewe hivyo tunajivunia suala hili na wakuu wa mikoa, makatibu Tawala na wakurugenzi nimewaomba mje hapa ili kutafsiri kwa vitendo kwenye ngazi za mikoa maana yapo mambo makubwa tunaweza kufanya, hivyo tumieni matamko ya viongozi na maono yao kufanya haya,”
Waziri Bashungwa amewataka viongozi hao kupeleka elimu waliyojifunza kwenye soko hilo kwenye maeneo yao na kuhakikisha wanawashirikisha machinga kwenye ujenzi wa miradi hiyo ambayo itatekelezwa kwenye mikoa yenye hadhi ya majiji nchini.
Na Angel Msimbira TAMISEMI
Wakuu wa Mikoa yenye Halmashauri zenye hadhi ya Majiji wametakiwa kutumia mbinu inayotumika katika ujenzi wa Soko la Wafanyabiashara wadogo (Machinga Complex) katika eneo la Bahi Road jijini Dodoma ili kuboresha zoezi la upangaji wa machinga kulingana na Mazingira ya maeneo yao.
Wito huo umetolewa Leo tarehe 12 Machi, 2022 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa wakati wa ziara yake na wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala, na Wakurugenzi wa mikoa yenye hadhi ya majiji kutembelea ujenzi wa eneo hilo.
Akizungumza na viongozi hao, Bashungwa alisema Rais Samia Suluhu Hassan ametambua sekta ya machinga kuwa rasmi hivyo kwa sasa wanaenda na maono yake ya kuhakikisha wanajengewa mazingira rafiki kwa kazi zao.
“Hapo awali changamoto ya machinga haikuwa na suluhu kwa sababu tuliyokuwa tunatafanya kuzitatua hayakuwa na uhalisia, hivyo kwa soko letu hapa baada ya maelekezo ya Rais kuwajengea mazingira rafiki tukaamua kutokwenda nje ya nchi kuiga wenzetu wanavyofana tukathamini vya ndani kwa kwenda eneo la Mnadani Msalato jijini hapa ili kuona ni namna gani watafanya biashara zao.
Napongeza ubunifu uliofanyika kwenye soko hili la machinga na namna jiji lilivyotafsiri maono ya Rais kwa kubuni masuala haya hii ni fursa kwa viongozi wengine wa mikoa yenye hadhi ya majiji kama Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya kujifunza kwa gharama ndogo hapa hapa nchini,” amesema Bashungwa.