Home » » DKT. YONAZI AMELIKUMBUSHA JESHI LA POLISI WAJIBU WA KUJIFUNZA NA KUTOA ELIMU YA USALAMA MTANDAO

DKT. YONAZI AMELIKUMBUSHA JESHI LA POLISI WAJIBU WA KUJIFUNZA NA KUTOA ELIMU YA USALAMA MTANDAO

Written By CCMdijitali on Monday, March 21, 2022 | March 21, 2022

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonaziakizungumza wakati akifungua mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi waMikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi (hawapo

pichani), yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) CP Camilius Wambura akizungumza wakati wa mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa,Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani),yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma

DKT. YONAZI AMELIKUMBUSHA JESHI 

LA POLISI WAJIBU WA KUJIFUNZA

 NA KUTOA ELIMU YA USALAMA 

MTANDAO

Na Faraja Mpina na Chedaiwe Msuya, WHMTH, DODOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi

amelikumbusha Jeshi la Polisi Tanzania kuwa linalo wajibu wa kujifunza na kuwaelimisha

wengine kuhusu makosa ya mtandao, namna ya kujilinda na kuchukua tahadhari dhidi ya

makosa ya mtandao.

 

Dkt. Jim ametoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya usalama mtandao kwa Wakuu wa

Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa madawati ya Upelelezi wa Jeshi la

Polisi kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar yanayofanyika kwa siku tano jijini

Dodoma kuanzia tarehe 21 Machi hadi tarehe 25 Machi, mwaka 2022

 

Amesema kuwa, Jeshi la Polisi linalo wajibu wa kujifunza kila siku, kwa kuwa wao pia ni

washirika katika ulimwengu wa mtandao kupitia matumizi ya simu janja lakini pia Wimbo wa

Jeshi la Polisi unasema wazi kuwa wana jukumu la kulinda usalama na haki za wananchi

ambapo utekelezaji wa jukumu hilo unafanyika katika ulimwengu mpya wa kidijitali.

 

“Dunia inabadilika kuna uhalifu mwingi unaofanyika kwa njia ya mtandao na watu wa

makundi yote kwa kukusudia au bila kukusudia, hivyo watendaji mnapopatiwa elimu mna

wajibu wa kuelimisha wengine kupitia nafasi za utendaji mlizo nazo sasa”, Amezungumza

Dkt. Yonazi

 

Ameongeza kuwa,“Ukimchapa mtoto lazima umfahamishe kwanini umemchapa na kosa ni

lipi, vivyo hivyo kwenye makosa ya mtandao, kabla ya kuyashughulikia ni vema wananchi

wapatiwe elimu na kufahamu makosa ya mtandao ni yapi”.

 

Dkt. Yonazi ameyazungumzia mafunzo hayo kuwa yanatoa taswira nzima na uelekeo wa

nchi katika kushughulikia masuala ya usalama mtandao ili kufikia malengo yanayotarajiwa

huku wajibu wa Wizara hiyo ni kuhakikisha mafunzo hayo ni endelevu na usalama katika

mtandao unasimamiwa vizuri.

 

Akizungumza na hadhira hiyo Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai nchini (DCI) CP

Camilius Wambura ameishukuru Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

kwa kuwezesha mafunzo hayo, kwa kuwa yatawasaidia watendaji wa Jeshi la Polisi

Tanzania kuongeza ujuzi utakaowafungua zaidi na kupanua wigo wa kupambana na uhalifu

hasa wa makosa mtandao.

 

“Teknolojia inabadilika kila kukicha hivyo mafunzo ya mara kwa mara kwa watendaji wetu

yanahitajika ili kuendana na kasi ya mabadiliko haya kwa watendaji kupitishwa wapi tulipo

na wapi tunaelekea katika kukabiliana na uhalifu wa mtandao”. Amezungumza Wambura

Naye Mkaribu Mwandamizi wa Polisi, SSP Joshua Mwangasa ameishukuru Serikali kupitia

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuwajengea uwezo watendaji

wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na hatua zinazoendelea za kuanza ujenzi wa maabara za

uchunguzi wa kisayansi zitakazojengwa kikanda katika mikoa sita ya Mbeya, Arusha

Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar ambazo zitasaidia kupanua wigo wa

uchunguzi wa makosa ya mtandao.

 

Mafunzo hayo ya usalama mtandao yanatolewa kwa watendaji wapatao 100 wa Jeshi la

Polisi Tanzania ikiwa ni muendelezo wa mafunzo yaliyotolewa mwezi Februari mwaka huu

kwa watendaji wa ngazi ya chini ya Jeshi hilo na sasa ni zamu ya wasimamizi wao ambao ni

Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi kama vile TAZARA na Bandari, Wakuu wa

Madawati ya Upelelezi wa Mikoa na Wakufunzi wa vyuo vya Polisi nchini.

 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, (DCP) Ally Lugendo akizungumza wakati wa mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani), yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma.


Mkaribu Mwandamizi wa Polisi, (SSP) Joshua Mwangasa akizungumza wakati wa mafunzo ya Usalama Mtandao kwa Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi na Wakuu wa Madawati ya Upelelezi wa Jeshi la Polisi yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (katikati), Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) CP Camilius Wambura (wa pili kushoto), Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, (DCP) Ally Lugendo ( wa kwanza kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Usalama Mtandao kutoka Jeshi la Polisi baada ya kufungua rasmi mafunzo hayo, jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Usalama Mtandao kutoka Jeshi la Polisi Tanzania,wakisikiliza kwa umakini hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya Usalama Mtandao iliyotolewa na Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,(hayupo pichani) yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Usalama Mtandao kutoka Jeshi la Polisi Tanzania,wakisikiliza kwa umakini hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya Usalama Mtandao iliyotolewa na Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,(hayupo pichani) yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma.


Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Usalama Mtandao kutoka Jeshi la Polisi Tanzania,wakisikiliza kwa umakini hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya Usalama Mtandao iliyotolewa na Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,(hayupo pichani) yaliyofanyika leo tarehe 21 Machi 2022, jijini Dodoma.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link