Home » , » MAFANIKIO YA AWAMU YA SITA MADARAKANI NDANI YA MWAKA MMOJA - WIZARA YA MADINI

MAFANIKIO YA AWAMU YA SITA MADARAKANI NDANI YA MWAKA MMOJA - WIZARA YA MADINI

Written By CCMdijitali on Thursday, March 10, 2022 | March 10, 2022


 YALIYOJIRI WAKATI WAZIRI WA MADINI DKT. DOTO BITEKO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA MAADHIMISHO YA MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA SITA MADARAKANI KATIKA SEKTA YA MADINI LEO MACHI 10, 2022

  • Chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, mchango wa Sekta ya Madini katika pato la taifa umekuwa ukiongezeka kutoka robo moja ya mwaka hadi nyingine
  • Katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2021 wastani wa mchango wa sekta hii umekuwa hadi kufikia asilimia 7.3 ya Pato la Taifa ikilinganishwa na wastani wa asilimia 6.5 Katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

 

  • Sekta ya Madini imeweka historia kwa kushuhudia mauzo ya moja kwa moja yenye thamani ya shilingi trillioni 8.3 kutokana na mauzo ya madini ya aina mbalimbali.
  • Wizara imekusanya shilingi bilioni 597.53 kama maduhuli ya Serikali.
  •  Ushiriki wa Watanzania kwenye shughuli za madini umekuwa kutoka asilimia 48 hadi asilimia 63 na hivyo kuongeza thamani ya huduma migodini kufikia thamani ya Dola za Marekani Milioni 579.3 sawa na Shilingi Trilioni 1.33.
  •  Wizara ya Madini imeanza ushirikiano na Wizara ya TAMISEMI ili kuweza kuwafikia wananchi wanaotumia madini hayo waweze kuchangia fedha zitokanazo na shughuli za uchimbaji madini kwa mujibu wa Sheria ya Madini.
  •  Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhesimiwa Samia Suluhu Hasan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kusimamia na kuhakikisha wachimbaji wadogo wanashiriki kikamilifu na kwa ufanisi kwenye uzalishaji madini hapa nchini.
  •  Katika awamu hii tumeshuhudia utoaji wa leseni mbalimbali kwenye shughuli za madini ukiongezeka.
  • Jumla ya leseni 8,172 zimetolewa, kati ya leseni hizo, leseni 5,937 ni za uchimbaji mdogo wa madini, leseni 282 ni za utafutaji wa madini, leseni 5 ni za uchimbaji wa kati wa madini, leseni 2 ni za uchimbaji mkubwa wa madini, leseni 49 ni za uchenjuaji wa madini, leseni 2 ni za usafishaji wa madini;
  •  Aidha leseni 1,531 ni za biashara ndogo ya madini na leseni 364 kubwa za biashara ya madini zilitolewa kwa wawekezaji na wananchi, ikilinganishwa na jumla ya leseni 6,334 zilizotolewa katika kipindi cha kuanzia Machi 2020 mpaka hadi Februari 2021.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link