|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisindikizwa na Mama Janeth Magufuli, Mjane
wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli, baada ya kuweka
shada la maua kwenye kaburi la hayati Dkt. Magufuli katika siku ya kumbukizi ya
mwaka mmoja ya kifo cha kiongozi huyo nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo
Machi 17, 2022.
Picha na Muhidin Issa Michuzi
|
|
Mama Janeth Magufuli, Mjane wa
aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli, akiaga wagen baada
ya hafla aliyoandaa kwa ajili ya kutoa misaada kwaya zenye uhitaji,
wafungwa pamoja na watoto yatima iliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita
leo Machi 18, 2022.
|
|
Mama
Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe
Magufuli, akipata picha ya kumbukumbu na watoto yatima wanaolelewa katika vituo
vya Ibn Ghanim cha Bwanga, Angel's Home cha Rulenge na Buseresere wakati
wa hafla aliyoandaa Mama Magufuli kwa ajili ya kutoa misaada kwa kwaya zenye
uhitaji, wafungwa , pamoja na watoto yatima iliyofanyika nyumbani kwake Chato
mkoani Geita leo Machi 18, 2022. |
|
Mama Janeth Magufuli, Mjane wa
aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli, akimbeba mmjoa wa
watoto yatima wakati wa hafla aliyoandaa Mama Magufuli kwa ajili ya kutoa
misaada kwa kwaya zenye uhitaji, wafungwa, pamoja na watoto yatima iliyofanyika
nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 18, 2022.
|
|
Mama
Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe
Magufuli, akimkabidhi misaada kwa wawakilishi wa kaya 100 wakati wa hafla
aliyoandaa Mama Magufuli kwa ajili ya kutoa misaada kwaya zenye uhitaji, wafungwa,
pamoja na watoto yatima iliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo
Machi 18, 2022. |
|
Mama Janeth Magufuli, Mjane wa
aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli, akimkabidhi misaada
kwa ajili ya wafungwa Mkuu wa Gereza la Chato Bw. Raphael Magesa wakati wa
hafla aliyoandaa Mama Magufuli kwa ajili ya kutoa misaada kwa kwaya zenye
uhitaji, wafungwa, pamoja na watoto yatima iliyofanyika nyumbani kwake Chato
mkoani Geita leo Machi 18, 2022. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Martha
Mkupasi na kati ni Mbunge wa Chato Dkt. Medard Kalemani.
|
|
Mama Janeth Magufuli, Mjane wa
aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli, akimkabidhi misaada
mwakilishi wa kituo cha kulelea yatima cha Ibn Ghanim wakati wa hafla
aliyoandaa Mama Magufuli kwa ajili ya kutoa misaada kwa kwaya zenye uhitaji,
wafungwa, pamoja na watoto yatima iliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita
leo Machi 18, 2022.
|
|
Mama Janeth Magufuli, Mjane wa
aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli, akimsikiliza Mbunge wa
Chato Dkt. Medard Kalemani, wakati wa hafla aliyoandaa Mama Magufuli kwa
kuikabidhi misaada kwa ajili ya kwaya zenye uhitaji, wafungwa, pamoja na watoto
yatima iliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 18, 2022.
|
MAMA JANETH MAGUFULI ATOA MISAADA KWA MAKUNDI YA WATU WENYE MAHITAJI CHATO
Mama Janeth Magufuli,
Mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli,
amesema ataendeleza utamaduni waliyojiwekea yeye na marehemu mume wake
wa kutoa misaada kwa wenye uhitaji wakati wa sikukuu za kidini ili
kugawana na wenzao kidogo walichojaaliwa nacho.
Mama
Magufuli ameyasema hayo wakati akikabidhi misaada mbalimbali kwa kwaya
100 zenye uhitaji, wafungwa, pamoja na watoto yatima katika hafla fupi
iliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 18, 2022.
Amesema
ameamua kutoa misaada hiyo katika kipindi hiki ambapo waumini wa dini
ya Kikristo duniani kote wako katika mfungo wa Kwaresima wa siku 40
ikiwa ni ishara ya kushiriki mateso pamoja na Yesu Kristo, aliyejitoa
sadaka kuteswa, kufa msalabani na baada ya siku tatu akafufuka ili
kumkomboa mwanadamu.
"Kipindi
cha Kwaresima ni cha kufunga na kufanya toba. kutafakari maisha yetu,
tujikane nafsi zetu kwa kutenda matendo mema na kujizuia kutenda vitendo
viovu ili kujisogeza karibu na Mwenyezi Mungu.
"Katika
kipindi hiki tunaaswa kiusaidia wenye uhitaji na shida mbalimbali kwani
(Mithali 19:17) Amhurumiayte masikini humkloipesha Bwana; Naye atamlipa
kwa tendo lake jema", alisema Mama Magufuli, ikiwa ni siku moja baada
ya kuadhimisha kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hjayati Dkt.
Magufuli iliyoongoza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan mjini Chato.
Misaada
alioyotoa ni pamoja na mchele tani 3.2, Maharage tani 3.4, sabuni za
miche za kufulia katoni 50 pamoja na sare za wanafunzi 500, ikiwa ni za
wasichana jozi 250 na idadi hiyo hiyo ya jozi kwa wavulana.
Hafla
hiyo ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Martha Mkupasi,
Mbunge wa Chato Dkt Medard Kalemani, Mkuu wa Gereza la Chato Bw. Raphael
Magesa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw. Batholomew Manunga
pamoja na viongozi wa dini, wadau wa maendeleo na wananchi.