Home » » MWELEKEO WA KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU BAADA YA MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA WABAINISHWA

MWELEKEO WA KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU BAADA YA MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA WABAINISHWA

Written By CCMdijitali on Sunday, March 20, 2022 | March 20, 2022

  




MWELEKEO WA KAZI, AJIRA, VIJANA NA 

WENYE ULEMAVU BAADA YA MWAKA

 MMOJA WA RAIS SAMIA WABAINISHWA


Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu imebainisha mipango mikakati ya kiutendaji katika majukumu inayoyaratibu ili kuhakikisha Maelekezo ya Mhe. Rais na Mhe. Waziri Mkuu yanatekelezwa kwa ufanisi na weledi katika kuboresha huduma za Ofisi hiyo, baada ya mwaka mmoja wa serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Akieleza mwelekeo wa Ofisi hiyo, kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, tarehe 20 Machi, 2022, Mhe. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Patrobas Katambi, amefafanua kuwa pamoja na kuwa Ofisi hiyo imetekeleza kwa mafanikio majukumu yake, hatua inayofuata ni kujikita katika tafiti katika masuala inayoratibu ya kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu.

Mhe. Katambi amefafanua kuwa Mhe. Rais amewataka waandae Programu maalum ya kutengeneza fursa za Ajira kwa vijana, ambapo Programu hiyo itahusisha Wizara, Idara, Wakala na Taasisi zote za serikali, Sekta Binafsi. Programu hiyo itahakikisha kuwa kila fedha inayotokana na serikali kwa hapa ndani au tunazozipata kutoka nje ya nchi, iweze kuzalisha fursa za ajira kwa vijana waliojiajiri au kutengeneza ajira. ” Amesisitiza Katambi

Ameongeza kuwa Programu hiyo itajikita pia katika katika miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali, ambapo utekezaji wa miradi hiyo utaweza kuzalisha ajira za moja kwa moja na ambazo sio za moja kwa moja.

Amefafanua kuwa mkakati mwingine ambao Ofisi hiyo iliyonao ni kuzitafuta Taasisi na wadau wa kimaendeleo watakao weza kutoa ruzuku, misaada pamoja na fedha zitakazo wawezesha vijana kujiajiri. Aidha, ameongeza kuwa wamejipanga kufanya Ufuatiliaji wa fedha zinazotolewa na halmashauri kwa ajili ya kuwakopesha Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu ambapo hadi sasa, zaidi ya shilingi bilioni 145.8 zimetolewa kote nchini.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link