Home » » WAZALISHAJI NCHINI WATAKIWA KURASIMISHA BIDHAA ZAO - WAZIRI KIGAHE

WAZALISHAJI NCHINI WATAKIWA KURASIMISHA BIDHAA ZAO - WAZIRI KIGAHE

Written By CCMdijitali on Friday, March 18, 2022 | March 18, 2022








 



  SERIKALI imetoa agizo kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini kurasimisha bidhaa zao

 na kutoa onyo kwa wale ambao watakao kwenda kinyume na agizo hilo.


Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa ziara ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira katika kiwanda cha Konyagi nchini (Tanzania Distillers Limited - TDL).

Mhe. Kigahe Amesema kuwa wazalishaji watakaozalisha bidhaa zisizorasimishwa watachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa wamekuwa wakiikosesha serikali mapato.

“Sisi kama Wizara tutahakikisha wale ambao wanazalisha nje ya utaratibu tutawasaidia warasimishe lakini wale watakaoendelea na uzalishaji wa bidhaa bandia watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kuwakamata na kuharibu bidhaa hizo, Tunautaratibu wa kusimamia wazalishaji ili wazalishe kwa tija na wasaidie uchumi wa nchi” ameeleza Mhe. Kigahe.


Kwa upande wake Mhe. David Kihenzile Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mbunge wa Mufindi Kusini, amesema kuwa kamati hiyo ipo kwenye zaira ya kutembelea viwanda, taasisi mbalimbali zinazohusu biashara na mazingira na kwamba wamefika kwenye kiwanda cha Konyagi cha TDL kwa ajili ya kuona uzalishaji na kusikiliza changamoto zao.

Amesema wamewasikia (TDL) wakidai kuwa takribani Asilimia 55 ya bidhaa zinazouzwa mitaani ni bandia.

Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa TDL Bi. Mesiya Mwangoka ameoimba Serikali kutengeneza adhabu ngumu zaidi ili wale wote wanaohusika na kutengeneza bidhaa bandia wasiweze kuendelea kufanya hiyo biashara.

"Tunaomba serikali kutunga sera kali zaidi kwani sera za sasa hivi zinamuwezesha yule anayetengeneza bidhaa bandia kuendelea na biashara yake, faini zake ni ndogo sana unakuta mtu anazalisha bidhaa bandia ya milioni mia mbili, faini yake analipa milioni mbili lazima aendelee kuzalisha kwa sababu haoni hasara kwa kuwa adhabu anayopewa ni ndogo sana na haimfanyi yeye kuvunja ile biashara", amesema Mwangoka.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link