WAZIRI MKENDA AAGIZA KUFANYIKA MKUTANO WA UCHAGUZI WA SKAUTI
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda ameteua kamati ya mpito ya watu watatu kusimamia shughuli za kiutendaji za Skauti nchini na Uchaguzi.
Waziri Mkenda ameteua kamati hiyo leo tarehe 18 Machi 2022 Jijini Dar es salaam wakati wa kikao kazi na kamati tendaji ya Skauti ambapo pia katika Kikao hicho alishiriki Skauti Mkuu Bibi Mwantumu Mahiza .
Wajumbe wa Kamati hiyo teule ni Bw Stewart Kiluswa, Omary Mavura pamoja na Suleiman Takadiri ambao wamepewa jukumu la kuhakikisha inaandaa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa uongozi wa Skauti
Waziri Mkenda ameitaka kamati hiyo ya mpito kuhakikisha kuwa inatoa Notisi ya Mkutano ifikapo tarehe 21 Machi 2022 huku akiagiza mkutano mkuu kufanyika ndani ya siku 21 baada ya tangazo hilo.