Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akipanda mti mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Tabi CCM Mwanambaya |
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mio wa Pwani, Ramadhani Maneno baada ya kuwasili patika ofisi za CCM Wilaya ya Mkuranga. |
Viongozi mbalimbali na wanachama wa CCM wakisimama kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM alipowasii katika ukumbi wa mkutano kwa ajili ya mkutano wa ndani wa Chama wilayani Mkranga. |
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara
Ndg Abdulrahman Omar Kinana amepokelewa wilaya ya Mkuranga leo tarehe 24
Aprili, 2022 kwa ajili ya ziara mkoa wa Pwani ya uimarishaji uhai wa
chama na kuhamasisha wana-CCM kujitokeza kushiriki uchaguzi wa ndani ya
Chama unaoendelea.
Akizungumza
na wanachama wa CCM ukumbi wa CCM wilaya ya Mkuranga Ndugu Kinana
amewataka wana-CCM kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi za uongozi ndani
ya Chama katika uchaguzi unaoendelea pamoja na kuwahimiza viongozi wa
ngazi zote kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa huru, haki na wenye
kuzingatia katiba ya CCM na kanuni zake ili kuwapata viongozi waadilifu.
"Viongozi
simamieni uchaguzi uwe huru na haki, acheni kubeba wagombea, epukeni
dhulma na chukueni hatua kwa kuwakata wale wanaotafuta uongozi au
umaarufu kwa fedha. Kwa kuwa tunataka uadilifu nje ya CCM basi ni lazima
tuanze kwanza sisi kuwa waadilifu." Amesema Kinana
Kinana
amesisitiza "Wana-CCM wanayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa lakini
haipo haki ya kununua au kununuliwa ili kupata au kutoa uongozi. Kuna
watu huwa hawana habari na chama wala wanachama wakati ambao sio wa
chaguzi ajabu wakisikia uchaguzi tu wanaanza kujipitisha kuwasalimu,
kugawa fedha na kuwachafua wengine tusiruhusu haya yajitokeze."
Aidha
Kinana amesema mahusiano mazuri baina ya CCM na serikali ni chachu ya
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM hali inayoimarisha imani ya
wananchi kwa Chama na serikali yao. Pia amewataka viongozi wa CCM
kuendeleza utamaduni wa kuwasikiliza wananchi na kuwasilisha changamoto
zao serikalini kwa utatuzi. Amehimiza wajibu huo ni walazima kwa sababu
ni CCM inayoomba kura na inayopigiwa kura.
Mapema
wakati wa Mapokezi Ndg Kinana ameshiriki uzinduzi wa ofisi ya tawi la
Mwanambaya kata ya Mipeko wilaya ya Mkuranga ambapo alichangia shilingi
milioni tatu kuunga mkono juhudi za Wana-CCM na viongozi wa tawi hilo za
kupata mazingira mazuri ya kufanyia shughuli za Chama.
Katika
ziara hii viongozi walioshiriki ni pamoja na mwenyeji wake Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Pwani Ndg Ramadhani Maneno, Kamati ya siasa ya mkoa wa
Pwani, kamati za siasa za wilaya zote za Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Mkoa wa
Pwani Ndg Abubakar Kunenge, wakuu wa wilaya zote, watendaji wote,
wabunge na madiwani wote wa Mkoa wa Pwani. Makamu Mwenyekiti wa CCM
Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omar Kinana ameondoka mkoa wa Pwani
kuelekea mkoa wa Tanga kuendelea na ziara yake akiwa ameambatana na
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu
Shaka.