Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe |
Waziri
wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe ameiagiza Bodi ya Korosho kuweka malengo
ya kuzalisha tani laki nne za Korosho kwa ajili kuuza nje ya nchi katika
msimu ujao wa uzalishaji.
Mhe. Bashe ameyasema hayo wakati wa
majumuisho ya mijadala kwenye kikao cha Tathmini ya Uzalishaji na
Masoko ya zao la Korosho kilichofanyika jijini Dodoma.
Aidha
Waziri Bashe ameagiza Bodi ya Korosho izalishe miche ya Korosho na
iisambaze kwa wakulima baadala ya kuwapelekea mbegu kwani wakulima
wengi hawana ujuzi wa kuzalisha miche.
Mhe. Bashe ameitaka Bodi
hiyo kuhakikisha inasimamia utaratibu wa mkulima mmoja kuzalisha mazao
manne kwa kuzingatia ikolojia za maeneo husika.
Mhe. Bashe
amesema endapo mkulima atazalisha mazao manne itamsadia kufanya
biashara ya mazao kila baada ya muda mfupi na kuwa na uhakika wa kipato
katika kipindi chote cha mwaka.
"Haiwezekani mkulima asubiri korosho ya mwezi wa kumi na aiuze mwezi wa kumi na mbili halafu utumie kipato hicho kutatua matatizo ya mwaka mzima." Amefafanua Mhe. Bashe.