MAJALIWA AITAKA TICTS KUIMARISHA
UTENDAJI KAZI
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia
Makontena Tanzania (TICTS) kuimarisha utendaji kazi wake ikiwemo kuacha
kuchelewesha ushushaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam.
Amesema
kuwa kampuni hiyo ina paswa kufanya kazi kwa weledi na kupitia mkataba
wa utendaji kazi wake ili kuhakikisha inatoa huduma stahili kwa wateja
wanaohudumiwa na bandari hiyo na kuwa kimbilio.
Ametoa agizo
hilo leo (Ijumaa, Aprili 08, 2022) jijiji Dar es Salaam wakati
alipozungumza na Viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka
ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Kampuni ya
Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) na kukagua utendaji
kazi wa Bandari ya Dar es Salaam kufuatia maagizo ya Rais Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
“Tunataka mrejesho mzuri kutoka kwa wateja wetu, bandari hii ndio injini ya uchumi wetu, hatutasita kufanya mapitio ya mkataba wa TICTS, wapo wawekezaji wengi ambao wana nia ya kuwekeza kwenye eneo hilo, hatuwezi kuvumilia kuona kuna ucheleweshwaji wa utoaji wa mizigo bandarini”
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Wizara itaendelea kuisimamia TPA ili kuhakikisha wanaendelea kupunguza zaidi na kwa wakati shehena yote inayopita kwenye bandari hiyo “Bandari ni sehemu muhimu kwenye uchumi wetu, tutahakikisha maeneo yote ambayo hayatumiki kuhifadhi mizigo yanaanza kutumika ili kuondoa msongamano”.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Eric Hamisi amesema kuwa wameendelea kufanya maboresho katika bandari hiyo ili kuongeza ufanisi ikiwemo kununua vifaa vipya kama vile Reach Stracker Saba (7) na FolkLift mbili (2) za tani 16 kila moja. @owm_tz