Home » » KIKAO KAZI CHA KUJENGA UHUSIANO MZURI KATI YA WAKAGUZI KATA, ASASI ZA SERIKALI NA ZISIZO ZA SERIKARI.

KIKAO KAZI CHA KUJENGA UHUSIANO MZURI KATI YA WAKAGUZI KATA, ASASI ZA SERIKALI NA ZISIZO ZA SERIKARI.

Written By CCMdijitali on Sunday, April 3, 2022 | April 03, 2022

 


 KIKAO KAZI CHA KUJENGA UHUSIANO 

 

MZURI KATI YA  WAKAGUZI KATA,

 

ASASI ZA SERIKALI NA ZISIZO ZA 

SERIKALI.


Leo tarehe 01.04.2022 katika ukumbi wa polisi Mabatini, ACP_ Mairi Wassaga ambaye ni Operesheni Ofisa Mkoa wa Mwanza amefanya kikao na wakaguzi Kata 37 toka Wilaya ya Nyamagana na Ilemela na wadau wa Asasi za serikali na kiraia.

ACP Makori akiwa ameambata na baadhi ya Maafisa amekaribishwa na SP- Dastani Kombe ambae ni Mkuu wa Ushirikishwaji Jamii Mkoa wa Mwanza, ambapo alieleza dhumuni la kikao hicho ni kutambulisha Wakaguzi Kata na Asasi hizo kwani wote wanakutana na Wananchi katika majukumu yao, hivyo ni muhimu kutambuana na kujua mipaka yao.

Aidha, alieleza kuwa baada ya kufahamiana watashirikiana katika shughuri mbalimbali za maendeleo katika ngazi ya Kata ambako ndio chimbuko la Maendeleo.

Kwa upande wao Wadau hao wameliomba Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza kuchukua hatua ili kukomesha ukatiri wa kijinsia na Makosa dhidi ya Binadamu kwani yameshamiri hususani kipindi hiki.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link