Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Abdulrahman Kinana |
Makamu Mwenyekiti mpya wa Chama cha
Mapinduzi CCM Abdulrahman Kinana leo amepokewa Jijini Dar es Salaam akitokea
Dodoma ambako hivi juzi alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti katika mkutano wa
CCM.
Ameyasema haya leo hii “Namshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu, nilikwenda Dodoma nikiwa Mwanachama wa kawaida nimerudi Makamu Mwenyekiti lakini ni kutokana na pendekezo lake, namshukuru kwa kuniamini, kuthamini mchango wangu kwa CCM na kuamini naweza kumsaidia"
"Nawashukuru Wana- CCM kwa kunichagua nawahakikishia nitafanya kazi kwa nguvu, kwa bidii, kwa uadilifu lakini vilevile nitajituma"
"Nitatanguliza utumishi na sio utukufu maana hivi karibuni hivi vyeo tunavyovipata nchini nikitazamatazama kuna mila na desturi inaanza ya vyeo kuendana na utukufu na mbwembwe nyingi, nataka nichukue nafasi hii kuwaomba wenzangu kwamba kuchaguliwa kupewa nafasi ya uongozi ni utumishi wa umma"
"Watakaotukuza ni wale unaowatumikia, ukifanya kazi vizuri watakutukuza, ukijitukuza mwenyewe watakushusha" ——— amesema Abdulrahman Kinana leo Jijini Dar es Salaam.