Mhe.Dorothy George Kilave Mbunge wa Jimbo la Temeke |
Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke Ndugu Kite Mfilinge |
MKUU wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo |
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Ndugu Almish Azar |
Meya wa Wilaya ya Temeke, Mheshimiwa Abdallah Chaurembo |
MHE. DOROTHY GEORGE KILAVE,
MBUNGE WA JIMBO LA TEMEKE,
AMETEKELEZA ILANI YA CCM KATIKA
MWAKA 2020/2021, KWA MAFANIKIO
LUKUKI JIMBONI
📝9Aprili 2022.
Mhe, Dorothy George Kilave, akiwa katika Mkutano Maalumu wa
Jimbo la Temeke, uliofanyika Siku ya Jana, Tarehe 9/04/2022 Katika Ukumbi wa
Mikutano wa IDDI NYUNDO Manispaa ya Temeke.
Mkutano huu, ulijumuisha Wajumbe kutoka Chama cha Mapinduzi
(CCM) ngazi ya Kata na Wilaya, Viongozi wa Vyama Vingine Vya Siasa, Pamoja na
Makundi Maalumu (Walemavu, walezi wa Vituo Vya Watoto na Wazee) Viongozi wa
Mashirika na Taasisi zisizo za Kiserikali na Baadhi ya Wafanyabiashara kutoka
Jimbo la Temeke.
Mhe Dorothy George Kilave, aliwasilisha Taarifa ya
Utekelezaji Kwa Mfumo wa Kitabu, Ambapo Kitabu hicho kina Kurasa 43 na Sura 7.
Msingi wa Kitabu hiki unasawili na kubainisha kile kilichoelekezwa katika ILANI
ya Uchaguzi ya 2020-2025, Ambayo imelenga zaidi kushughulika na Kero,
Changamoto Mbalimbali za Watanzania ili kuboresha Maisha na huduma, Kwa Ustawi
wa Jamii.
Mkutano wa Uwasilishaji wa ILANI ya CCM Kwa Mwaka Mmoja Jimbo
la Temeke umehudhuriwa na Viongozi wa Chama na Serikali Ndani Wilaya ya Temeke.
Mhe.Dorothy George Kilave Mbunge wa Jimbo la Temeke,
amewahakikishia kuwa kama alivyo anza, ataendelea kutekeleza Kwa zaidi ya
ubora, Katika Kila hatua ya Mwaka Mmoja wa Utekelezaji wa Maelekezo ya CCM
katika Kuwahudumia Wananchi wa Jimbo la Temeke.
Lengo ni Kuboresha na kuimalisha Maisha ya Wananchi wa Jimbo
la Temeke Kwa kutoa huduma iliyo Fanisi Kwa Matarajio ya Pamoja.
Pia, Mhe.Dorothy George Kilave Mbunge Temeke, Kupitia Ndugu,
Bi Almish Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke ambaye alimwakilisha Ndugu, Mama
Kate Kamba M/kiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam katika Ugeni Rasmi wa Mkutano,
Alikabidhi "Vyeti Vya Pongezi Kwa Wajumbe wa Kamati ya Fedha ya Mfuko wa
Jimbo" Kwa ushirikiano walioutoa katika Shughuli za Jimbo kupitia Kamati.
Wajumbe wa Mkutano na Wageni waalikwa wamempongeza Sana Mhe Mbunge wa Jimbo la Temeke Kwa kutekeleza ILANI ya CCM Kwa weledi Mkubwa.
"MENGI YAMEELEZWA KATIKA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI
YA CCM KWA MWAKA MMOJA NDANI YA JIMBO LA TEMEKE."
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Temeke