Naibu
Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa
MKATABA UTAFITI WA GESI YA HELIAM WASHUHUDIWA
Naibu
Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameshuhudia utiaji Saini Mkataba
wa Utafiti wa Gesi ya Helia bym kati ya Kampuni ya Noble Helium Limited
kupitia Kampuni yake Tanzu ya Rocket Tanzania Limited na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam kwa ajili ya Utafiti wa Gesi ya Heliam katika maeneo
mbalimbali nchini.
Utafiti huo, utahusisha maeneo manne tofauti
ikiwemo eneo la Ziwa Nyasa, Ziwa Eyasi, Ziwa Rukwa pamoja na Ziwa
Manyara ambapo mradi huo utaajiri wafanyakazi wake wote kutoka Tanzania
na wafanyazi wasiozidi kumi watatoka nje ya nchi.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Dkt. Kiruswa amesema viashiria vya uwepo wa gesi ya
heliam katika maeneo mbalimbali ya nchi ni uthibitisho tosha unao onesha
kubarikiwa kwa nchi ya Tanzania, kwani ni madini ambayo yanategemewa
kuongeza Pato la Taifa kwa kuwa yanahitajika sana kwenye shughuli za
uchumi wa kileo.
Pia, Dkt. Kiruswa ameishauri Kampuni ya Rocket
Tanzania Limited kuishirikisha Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini
Tanzania (GST) kwa kuwa ina taarifa nyingi za awali za uwepo wa madini
katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) sababu shirika hilo linafanya shughuli za utafiti wa madini na
lina vifaa vya kutosha vya utafiti.
"Naomba nichukue fursa hii kumpongeza Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake mazuri anayotupa sisi wasaidizi wake, anataka kuona mazingira ya uwekezaji nchini yanakuwa bora na ya kuvutia," amesema Dkt. Kiruswa.
Imeelezwa kuwa, uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki hususan kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, pia heliam hutumika katika teknolojia ya kutengeneza vifaa vya maabara, roketi, mitambo ya kinyuklia, vifaa vya elektroniki na vifaa vingine vingi.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye amempongeza Naibu Waziri kwa kukubari kuja kushuhudia utiaji saini wa mkataba huo ambapo amesema mradi hou utainufasha Tanzania kwa kuongeza pato la taifa na kuongeza ajira kwa watanzania.