RC MAKALLA; TANZANIA TUNA MAFUTA
YA KUTOSHA KUTUMIA MPAKA JULY 15.
- Ni Mafuta yaliyopo Sasa na Yale yaliyopo kwenye Meli.- Asema Hakuna uhaba wowote wa Mafuta nchini kwa mafuta ya Dizel, petrol, mafuta ya Taa Na Ndege.- Ampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka Mpango mzuri uliowezesha Nchi kuwa na akiba ya kutosha.- Atangaza matokeo ya kamati ya uchunguzi juu ya wezi waliochepusha mafuta bomba kuu kuwa walikamatwa na wako mikononi mwa vyombo vya sheria.- Bomba lipo Salama Baada ya kufukuliwa lote na kufukiwa upya, chombo Cha kufuatilia usalama wa bomba kinunuliwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema kiasi cha akiba ya
nishati ya mafuta kilichopo Sasa na yale yaliyopo kwenye Meli
yakishushwa yatatosha kutufikisha mpaka July 15 mwaka huu hivyo hakuna
sababu yoyote ya Wananchi kuwa na hofu.
Hayo
ameyasema leo jijini Dar es salaam alipokutana Na wadau wa mafuta Na
wakala wa uagizaji mafuta pamoja kwa lengo la kutoa mrejesho wa kamati
ya uchunguzi wa wizi wa mafuta Na kupokea taarifa ya hali ya mafuta
nchini.
Aidha RC Makalla
amesema kiasi Cha Mafuta yaliyopo Sasa ukijumlisha na Yale
yatakayoshushwa na Meli yatafanya Nchi kuwa na akiba ya Lita Milioni
512.7 za Dizeli, Petrol Lita Milioni 365.5, Mafuta ya ndege Lita Milioni
40 na Mafuta ya taa Lita Milioni 5.9 ambapo kwa pamoja yanaweza
kutumika mpaka July 15 mwaka huu.
Kutokana
na Mkoa wa Dar es salaam kuwa lango kuu la Biashara ya mafuta, RC
Makalla amesema Serikali itaendelea kulinda na kudhibiti Miundombinu ya
Mafuta ili kutokomeza tatizo la Wizi na uchepushaji wa Mafuta na usalama
wa Wananchi ambapo amesema kwa Sasa Bomba la Mafuta lipo salama.
Hata
hivyo RC Makalla ametoa Matokeo ya Kamati aliyounda kuchunguza Wizi wa
Mafuta kutoka bomba kuu ambapo amesema zaidi ya watu 15 walikamatwa na
wapo Chini ya Vyombo vya sheria na kueleza kuwa tayari Serikali
imefanyia kazi mapendekezo ya Kamati ikiwa ni pamoja na kufukua upya
Bomba la Mafuta na kulifukia na ununuzi wa kifaa Cha kutambua wapi
Bomba limechepushwa.
Kuhusu
suala la foleni za malori Bandarini zinazosababishwa na upanuzi wa
Barabara, RC Makalla ameelekeza Shughuli za Ujenzi kufanyika
pasipokuathiri Shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja Ujenzi barabara ya
kuingia Na kutoka bandarini kufanyika usiku.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wakala wa uagizaji Mafuta kwa pamoja
Erasto Simon na Wadau wa Mafuta kwa pamoja wamemshukuru RC Makalla kwa
hatua za haraka alizochukuwa kudhibiti tatizo la Wizi na uchepushaji wa
Mafuta lililokuwa limedumu kwa muda mrefu na Sasa wanakiri kupokea kiasi
Cha Mafuta sawa na kile walichoagiza.