Naibu
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete,
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete, amesema ili kuondokana na changamoto ya upungufu wa mabehewa, Shirika la Reli Tanzania (TRC), inakarabati mabehewa 37 ili kuimarisha huduma ya usafiri wa treni mkoani Kigoma.
Mhe. Mwakibete alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Kilumbe Ng’enda, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuboresha usafiri wa Reli ya Kigoma – Dar es Salaam ambao umekuwa ukifanya safari mbili kwa wiki badala ya safari moja kila siku kama ilivyokuwa awali.
Naibu Waziri Mwakibete, amelihakikishia Bunge kuwa Serikali inaendelea na zoezi la ukarabati na ununuzi wa mabehewa ya abiria na baada ya utekelezaji wa kazi hizo, idadi ya safari za treni kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma zitaongezeka kutoka safari mbili hadi nne kwa wiki.
@bunge.tanzania
@kigomars
@tzrailways