Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya |
BARABARA YA MWANZA – SHINYANGA
KUKARABATIWA
Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya, amesema Serikali imeanza maandalizi ya ukarabati wa barabara kuu ya Mwanza – Shinyanga yenye urefu wa kilometa 104 ambao utahusisha upanuzi wa barabara hiyo kutoka njia mbili hadi njia nne sehemu ya Mwanza Mjini – Usagara yenye urefu wa kilometa 25.
Akijibu swali Bungeni leo lililoulizwa na Mbunge wa Nyamagana, Mhe. Stanslaus Mabula, Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Kasekenya amesisitiza kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa barabara hiyo iko katika hatua za mwisho na inatarajiwa kukamilika baadae mwezi huu.
Amesema baada ya usanifu wa kina kukamilika na gharama za ukarabati kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ukarabati utakaohusisha upanuzi wa barabara hiyo.
@bunge.tanzania
@mkoamwanza