TANZANIA NA INDIA KUIMARISHA
UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA
Tanzania
na India zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika utoaji wa huduma
za tiba baina ya nchi hizo mbili kupitia Hospitali ya Apolo yenye makao
makuu nchini India.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi wakati wa kikao na Makamu
wa Rais anayeshughulika na Ukuaji wa Biashara wa Hospitali ya Apollo, Bw
Radhey Mohan.
Prof. Makubi amesema kuwa katika mazungumzo yao
wamekubaliana kukuza ushirikiano uliopo katika masuala ya kubadilishana
uzoefu katika utoaji wa huduma za tiba.
Aidha, Prof. Makubi
amemshukuru Bw. Mohan kwa kuwapatia matibabu bora Watanzania wanaopewa
Rufaa ya kutibiwa katika Hospitali za Apollo zilizopo nchini India.
Aidha Serikali inaendelea kuimarisha huduma za kibingwa ili watalaamu
waweze kuzitoa hapa hapa nchini .
"Tunawashukuru kwa kuwezesha utoaji wa mafunzo ya huduma kibingwa na ubingwa bobezi kwa wataalam kutoka Hospitali za Taifa pamoja na matibabu kwa watanzania tunaowapa rufaa kuja kutibiwa kwenye hospitali yenu".
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Hospitali ya Apollo Bw. Mohan aliishukuru Wizara ya Afya kwa kuendelea kuiamini Hospitali hiyo na kupeleka wagonjwa wanaohitaji matibabu ambayo hayapatikani hapa nchini.
Bw.Mohan ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali wakati wowote unapohitajika...
#AfyaKwanza
#JaliAfyaYako