Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mainduzi CCM Daniel Chongolo amewahakikishia wajumbe
wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama hicho Taifa wakiongozwa na Mwenyekiti
wa Chama hicho Samia Suluhu Hassan kwamba kwa kushirikiana na
sekratarieti ataendelea kutekeleza majukumu makubwa ya Chama katika
nafasi ya utendaji aliyonayo.
Chongolo amesema hayo leo Aprili 1
mwaka huu mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa ambapo
amesema leondio mara yake ya kwanza kusimama kwenye Mkutano huo tangu
alipoteuliwa Katibu Mkuu.
Kabla ya kuwasilisha maelezo kuhusu
Mkutano Mkuu maalum,Chongolo ametumia nafasi hiyo kueleza leo ndio mara
yake ya kwanza kabisa kusimama mbele ya mkutano mkuu wa CCM Taifa akiwa
Katibu Mkuu Taifa ,hivyo akaomba kueleza machache.
"Kwanza
kabisa namshuru Mungu kwa kutujaalia neema yaa uhai na afya njema na
leo tunakutana hapa.Naomba kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM
taifa kwa uamuzi wenu wa busara mlioufikia kwenye ukumbi huu wa Jakaya
Kikwete siku ya Aprili 30 ya mwaka 2021 kwa kumchagua tena wa kura zote
mpendewa wetu Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan kuwa Mwenyekiti wetu.
"Tatu namshukuru sana Mwenyekiti
wangu na Mwenyekiti wa Chama chetu ndugu Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi
wake wa kupendekeza jina langu mara baada ya kumaliza kwa Mkutano Mkuu
wa CCM Taifa ili nichaguliwe kushika nafasi kubwa ya utendaji katika
chama chetu
"Aidha kwa mara nyingine tena ninawashukuru wajumbe
wote wa Halmashauri Kuu Taifa kwa uamuzi wao wa kukubali kunichagua kuwa
Katibu Mkuu, Mimi na wajumbe wenzengu wote wa sekretarieti
tutahakikisha tunatekeleza majukumu yetu.
"Kwa hakika Chama hiki
kikubwa ambacho sio tu kina wachama ,wapenzi na wakereketwa wengi
kushinda chama kingine chochote cha siasa nchini Tanzania bali kinabeba
matumaini ya waliyo wengi na kwa ridhaa ya wananchi kitaendelea kuwa
dhamana kwa muda mrefu ili kilete maendeleo katika nyanja zote zote za
maisha ya binadamu,"amesema Chongolo.
Amesisitiza kuwa kwa
kuzingatia ukweli huo amemhakikishi Mwenyekiti wa Chama hicho na Wana
CCM wote kuwa hatawaangusha."Ninapenda kuwathibitishia wajumbe wa
mkutano mkuu taifa pamoja na wana ccm wote kwa kushirikiana na wezangu
nitatekeleza majukumu yangu ya ujenzi wa Chama chetu kwa bidii, nidhamu
na weledi mkubwa."
Kuhusu Mkutano Mkuu Maalum wa Chama
hicho,Chongolo amesema kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CCM inaeleza
mkutano mkuu WA CCM Taifa utafanya mikutano mitatu kila baada ya miaka
mitano, mikutano miwili kati ya hiyo itakuwa ya uchaguzi na mmoja
utakuwa wa kazi.
Ameongeza kalenda ya vikao vya Chama itaeleza ni
lini mikutano hiyo inafanyika , lakini mkutano usiokuwa wa kawaida
unaweza kufanyika wakati wowote ukiitishwa na Mwenyekiti wa CCM au
ukiombwa na theluthi mbili ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM
Taifa."Taarifa ya kukutana kwa mkutano huo unatakiwa kutolewa si chini
ya miezi miiwili kabla ya tarehe ya kukutana lakini inaweza kutolewa
muda mfupi zaidi huo wa kawaida."
Home »
KITAIFA
» ALIYOYASEMA KATIBU MKUU CCM DANIEL CHONGOLO MBELE YA WAJUMBE MKUTANO MKUU MAALUM...AMSHUKURU RAIS SAMIA
ALIYOYASEMA KATIBU MKUU CCM DANIEL CHONGOLO MBELE YA WAJUMBE MKUTANO MKUU MAALUM...AMSHUKURU RAIS SAMIA
Written By CCMdijitali on Friday, April 1, 2022 | April 01, 2022
Labels:
KITAIFA