Wafugaji wa nyuki katika halmashauri ya Wilaya ya Itigi Mkoani Singida wamepatiwa mafunzo ya ufugaji wa nyuki Ili kuongeza uzalishaji na tija katika kuongeza thamani mazao ya nyuki kupitia mradi wa EIF TIER II.
Awali
akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Idara ya Utawala na Maendeleo ya
Rasilimali watu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Edward
Nkembo Amesema kuwa anawashukuru wafugaji wote waliofika Kwa ajili ya
kupatiwa mafunzo ya mnyonyoro wa thamani wa asali Mkoani Singida.
Bw.
Nkembo Amesema kuwa mafunzo haya ambayo yataendeshwa na Shirika la
kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Singida kupitia mradi wa
Enhanced Intergrated Framework (EIF) ambao ni mradi wa kuwajengea uwezo
wajasiriamali wadogo na wa kati walioko katika mnyororo wa thamani
katika mazao ya Asali Mkoa wa Singida, Mawese Kigoma, Mbogamboga na
matunda kwa Mkoa wa Mara na Simiyu pamoja na Mwani na Dagaa Kwa Tanzania
Visiwani.
"Serikali kupitia mradi huu wa Enhanced Intergrated Framework (EIF) umedhamiria kujenga Viwanda Viwili vidogo katika kata za Mwamagembe na Itigi pamoja na kuwawezesha wajasiriamali kupata mizinga ya kisasa ya kuvunia asali kupitia vikundi vyenu". Amesema Bw. Nkembo.
Bw. Nkembo ameongeza kwa kusema kuwa Viwanda hivyo vitasaidia kusindika asali kwa ubora na Viwango vya kimataifa na kuyafikia zaidi masoko ya ndani na nje ya nchi.
Awali akielezea utekelezaji wa mradi wa kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wa kati Kaimu mratibu na Msimamizi wa mradi wa EIF TIER II kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bi. Natasha Ngowi amesema mafunzo hayo yamelenga kuwaelimisha wajasiliamali hao kuhusu uchakataji na usindikaji wa zao la asali
na uongezaji thamani wa bidhaa nyinginezo zitokanazo na nyuki.
Bi. Natasha amesema kuwa lengo jingine la mradi huu ni kuimarisha ushindani wa Biashara ndogo na za kati Ili kuyafikia masoko ya ndani na ya kimataifa, kupunguza umaskini na kutoa ajira kwa Wanawake na Vijana.
Bi. Natasha ameongeza kwa kusema kuwa mradi huu unafadhiliwa na chombo kinachoitwa Enhanced Integrated Framework (EIF) ambacho kipo katika shirika la Biashara la Dunia (WTO), UNDP na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ufadhili wa mradi huo.