Home » , » TANZANIA NA UINGEREZA ZIKUBALIANA KUWEKA MIKAKATI YA PAMOJA KUPAMBANA NA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU WAKIWEMO WATOTO.

TANZANIA NA UINGEREZA ZIKUBALIANA KUWEKA MIKAKATI YA PAMOJA KUPAMBANA NA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU WAKIWEMO WATOTO.

Written By CCMdijitali on Monday, April 4, 2022 | April 04, 2022


TANZANIA NA UINGEREZA ZIKUBALIANA KUWEKA MIKAKATI YA PAMOJA KUPAMBANA NA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU WAKIWEMO WATOTO.

 WMJJWM- Dar Es Salaam

Tanzania na Uingereza zimekubaliana kuweka mikakati ya pamoja kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu wakiwemo watoto hasa maeneo ya
mipakani.

Hayo yamebainika tarehe 04 Apr2022 jijini Dar Es Salaam wakati wa ziara ya Waziri wa Uingereza anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mhe. Vicky Ford iliyolenga kujadiliana na kutafuta suluhu ya tatizo la usafirishaji haramu wa binadamu wakiwemo watoto.

Akizungumza mara baada ya ziara
kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Zainab Chaula amesema, Uingereza imetoa jengo Maalum kwa ajili ya kutoa huduma za pamoja kwa ajili ya kusaidia waathirika wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kupata huduma za Afya, ushauri wa kisaikolojia, Msaada wa kisheria na huduma za Polisi katika eneo moja ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha suala hilo linapatiwa ufumbuzi uwajibikaji wa pamoja unahitajika kwa wataalam mbalimbali wanaohusika na kusaidia waathirika wa vitendo vya ukatili ili kusaidia kutoa huduma stahiki kwa uharaka na urahisi kwa kuokoa Jamii.

"Huduma hizi zitapatikana hapa hapa katika eneo moja na hasa kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza tumekusudia kubadili mazingira na kuleta huduma za pamoja kwa wahanga wa vitendo vya ukatili katika jengo la British Council na hii itakuwa ni kwa kuanzia na maeneo haya yatasambaa kila Mkoa" alisema Dkt. Chaula

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Waziri wa Uingereza anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Mhe. Vicky Ford amesema tatizo la usafirishaji haramu wa watu inaongezeka kwa kasi hasa katika mipaka hivyo kutishia ustawi wa jamii hasa watoto.

Mhe. Vicky ameeleza kuwa Uingereza ipo tayari kushirikiana na Tanzania hasa katika kuweka Mipango mikakati ya kuhakikisha tatizo la usafirishaji haramu wa watu hasa Watoto linapungua "

"Usafirishaji haramu wa watu ni tatizo kubwa hasa kwa Nchi za Afrika ambazo zimekuwa njia ya kusafirisha watu kuenda nchi za Ulaya. Tudhibiti hili tuiokoe jamii yetu" alisema Mhe








Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link