Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria Bw. Ahmed Djellal katika ofisi za Wizara jijini Dodoma. |
WAZIRI UMMY AOMBA WAWEKEZAJI WA
BIDHAA ZA DAWA KUTOKA ALGERIA
Waziri
wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi
wa Algeria Bw. Ahmed Djellal katika ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Pamoja
na mambo mengine, Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya Algeria kwa
udhamini wa mafunzo ya wataalam mbalimbali wa Afya nchini Algeria
Waziri
Ummy amemuomba balozi huyo Serikali yake kuendelea kutoa ufadhili kwa
watanzania hususan katika sekta ya afya katika fani za kibingwa na
bobezi katika upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu, Radiolojia na
Wataalam wa Usingizi.
Aidha, Waziri Ummy amemuomba balozi huyo
kuhamasisha wawekezaji wa viwanda vya dawa kutoka Algeria kuja kuwekeza
nchini Tanzania kwani nchi hiyo inazalisha asilimia 70 ya bidhaa za
dawa.