Home » » MAKAMU WA PILI WA RAIS-MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

MAKAMU WA PILI WA RAIS-MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

Written By CCMdijitali on Sunday, September 11, 2022 | September 11, 2022

 ………………………PRESS RELEASE…………………..
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wazazi, walezi wenyeviti wa skuli pamoja na walimu wakuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kushirikiana ili kuondosha tatizo kufeli kwa wanafunzi wa mkoa huo.


Mhe. Hemed ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na wazazi, walezi pamoja na walimu wakuu wa skuli za Maandalizi, Msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi Kwa Mkoa wa kaskazini Unguja katika kikao cha kuimarisha utendaji kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni.


Ameeleza kuwa wazazi na walezi kwa kushirikiana na walimu wakuu ndio wasimamizi wakubwa kwa wanafunzi ambapo ushirikiano wao unapelekea kupata wataalamu bora ambao watalisaidia taifa hapo
baadae.


Aidha makamu wa pili w rais ameutaka uongozi wa mkoa wa kaskazini unguja kushirikiana na wizara kutumia mbinu mbadala ili kuweza kuondosha kufeli kwa wanafunzi.


"kiujumla matokeo ya wanafunzi kwa mkoa wa kaskazini hayapo vizuri ukilinganisha na mikoa mengine, lazima wazazi, walezi, walimu wakuu na vingozi wa mkoa tushirikiane ili kuondosha wimbi hili la kufeli kwa wanafunzi wetu kila mwaka” Amesema


Akizungumzia suala la uhamisho kwa walimu mhe. Hemed ameutaka uongozi wa mkoa kwa kushirikiana na wizara ili kukabiliana na tatizo la uhamisho wa walimu kiholela jambo ambalo linasababisha kushuka kwa kiwango cha elimu.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameutaka uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhakikisha katika ajira zilizotangazwa hivi karibuni kunakuwa na uwiano wa walimu kwa mujibu wa mahitaji halisi ili kuondosha tatizo la mlundikano wa walimu katika eneo moja na maeneo mengine kuendelea kuwa na uhaba.


Aidha Mhe. Hemed ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Dkt. Hussen Ali Mwinyi itahakikisha inatoa ushirikiano wa kutosha kwa walimu ili kuboresha mazingira ya
kiutendaji.


“ Serikali imeamua kuboresha maslahi kwa watumishi wake wakiwemo walimu ili kuweza kufanya kazi kwa weledi mkubwa na kuhakikisha wanapatikana wataalamu na viongozi bora wa hapo baadae” amesema.


Pamoja na mambo mengine Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameutaka uongozi wa wizara hio kuhakikisha wanafatili maendeleo ya walimu wa skuli zote za serikali na binafsi ili kuweza kuzalisha
wataalamu wa kila sekta.


Nae katibu mkuu wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Khamis Ali Juma amesema kuwa wizara imejipanga kutatua changamoto zote zinazowakabili walimu ikiwemo kulipwa feza zao zote hasa walimu waliotoka kwenye ugatuzi.


Aidha amewataka walimu wakuu,wazazi na walezi kushirikiana pamoja kuzisimamia kambi za wanafunzi wakati wa kujiandaa na mitihani ya taifa.


Kwa upande wao walimu wakuu wa skuli za Mkoa wa Kaskazini Unguja wameiomba Serikali kuondosha changamoto zote zinazowakabili ikiwemo uchakavu wa majengo, ubovu wa barabara,uhaba wa vitendea kazi pamoja na kulipwa stahiki zao ili kufanya kazi kwa weledi kwa Maslahi ya taifa.


WAKATI HUO HUO MAKAMU WA PILI WA Rais amekutana na madaktari na wahudumuwa afya wa mkoa wa kaskazini Unguja katika ukumbi huo huo wa chuo cha mafunzo ya amali Mkokotoni na kusema kuwa serikali itahakikisha inaboresha maslahi ya madaktari kwa mujibu wa sheria.
Mhe. Hemed amesema kuwa serikali ya awamu ya Nane itahakikisha inaboresha maslahi ya madaktari pamoja na kuimarisha mazingira ya ufanyaji wa kazi.


Aidha Makamu wa Pili wa Rais ameutaka uongozi wa mkoa kushirikiana na wizara pamoja na utumishi wa umma kuhakikisha madaktari ambao wataajiriwa wanatoka sehemu husika ili kuboresha
ufanisi wa kazi.


Mhe. Hemed amewataka wataalamu hao kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa wanaofika hospitalini na kutoa huduma bora.
Amesema Serikali inathamini sana mchango wa madaktari hivyo amewataka kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa maslahi ya taifa na kuahidi kuwa changamoto zote zinazoikabili sekta ya afya serikali
itazitafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo.


Kwa upande wake waziri wa Afya Mhe.Nassor Ahmed Mazrui amesema kuwa uongozi wa Wizara ya Afya umejipanga kuboresha miundombinu ya kila hospitali ili kufikia malengo ya serikali
iliyojiwekea ya kutoa huduma bora kwa kila mwananchi.
Mhe.Mazurui amesema kuwa Serikali itajenga ofisi za madktari wilaya (DMO) ili kuleta ufanisi katika kazi zao pamoja na kuwapatia vitendea kazi.

Nao madaktari wa mkoa huo wameiomba Serikali kuweka vifaa vya uhakika vya matibabu pamoja na kuimarisha miundombinu iliyopo ili kutoa huduma bora kwa kila mwananchi anaefika kufata huduma katika kituo cha afya husika.

………………
OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS
11.09.2022
Ali Moh’d






 

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link