RC MAKALLA AMALIZA SINTOFAHAMU YA STENDI YA MAGUFULI NA STENDI BINAFSI.
- Awataka LATRA kutokwepa majukumu Na nyaraka zao walizotoa kwa stendi binafsi.
-
Aruhusu stendi binafsi 5 zilizohakikiwa Na LATRA kuendelea kutoa huduma
Kwa sharti la kuingia na kutoka wapitie stendi Magufuli.
- Aagiza Manispaa ya Ubungo kukaa Na wamiliki wa stendi binafsi kuona njia bora kukusanya mapato.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametangaza kuondoa katazo
lililokuwa likizuia Mabasi yaendayo mikoani na nje ya Nchi kutoruhusiwa
kupakia abiria au kushusha katika Vituo binafsi na badala yake ameruhusu
utaratibu huo kuendelea Kwa sharti la kila basi kuingia ndani ya Kituo
kikuu Cha Mabasi Cha Magufuli.
RC
Makalla ametoa maamuzi hayo wakati wa kikao Cha pamoja baina ya LATRA,
Wamiliki wa Stendi binafsi na Halmashauri ya Ubungo na kubaini
pasipokuwa na shaka kuwa Waliotengeneza Vituo binafsi walifuata taratibu
na kupatiwa Vibali na LATRA
Baada ya kukidhi vigezo.
Miongoni
mwa vigezo vilivyotolewa na LATRA ili kuruhusiwa kuanzisha Stendi
binafsi ni pamoja na uwepo wa Vyoo, Sehemu ya mapumzimo kwa abiria,
viburudisho Na sehemu ya maegesho.
Kutokana
na Hilo RC Makalla ameridhia Vituo binafsi 5 vilivyohakikiwa kuendelea
kutoa huduma na kufungua milango kwa wamiliki wengine wanaohitaji kuwa
na Vituo binafsi kushirikiana na LATRA ili wapatiwe vigezo
vinavyohitajika ambapo wamepewa Mamlaka ya kufuta au kutoa leseni.
Aidha RC Makalla ameagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kukaa kikao
Mara moja na wamiliki wa Stendi binafsi ili kuona njia Bora ya ukusanyaji wa mapato.