Home » » Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato imepokea bilioni 18 kwa ajili ya vifaa tiba vya kisasa kama CT - scan, MRI, Thioroscope na ECHO

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato imepokea bilioni 18 kwa ajili ya vifaa tiba vya kisasa kama CT - scan, MRI, Thioroscope na ECHO

Written By CCMdijitali on Thursday, October 13, 2022 | October 13, 2022

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA - CHATO YAPOKEA BILIONI 18 ZA VIFAA TIBA

Waziri wa Afya, @ummymwalimu amesema Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato imepokea bilioni 18 kwa ajili ya vifaa tiba vya kisasa kama CT - scan, MRI, Thioroscope na ECHO kwa ajili ya uboreshaji huduma za afya kanda ya Ziwa.

Waziri Ummy amebainisha kauli hiyo leo wilayani Chato mkoani Geita wakati akikagua maandalizi ya kuweza kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani anayetarajia kutembelea Hospitali hiyo siku ya Jumamosi Tarehe 15 Oktoba, Mwaka huu. 

Akizungumza Mhe. Ummy ameeleza kuwa hospitali hiyo itahudumia wagonjwa kutoka mikoa ya Jirani ili kupunguza mzigo mkubwa kwa Hospitali ya Bugando na Wizara ya Afya wataipa kipaumbele kwa kuhakikisha kila kinacho hitajika katika hospitali kinapatikana kwa haraka kwa umuhimu wa hospitali hiyo.

MWISHO












Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link