Zoezi la makabidhiano, limehudhuriwa na Viongozi wa CCM ngazi ya matawi na Kata, Pamoja na Uongozi wa Serikali ngazi ya Mtaa na Kata wakiongozwa na Mhe Diwani wa Kata ya Azimio.
Mhe Mbunge, amesisitiza kwamba ataendelea kuunga mkono Juhudi zinazofanywa na Viongozi, Wananchi na Jeshi la Polisi katika kuimalisha ulinzi na usalama Ndani ya Jimbo la Temeke na Temeke Kwa ujumula, lengo letu tunahitaji Vituo Hivi viwebora na vifanye kazi masaa24.
Pia, ameshukuru kazi kubwa inayofanywa na Askari Polisi, katika Swala la ulinzi, huku akiwasisitiza Sana, Wananchi kutoa Taarifa panapokuwa na viashiria Vya uhalifu na kuongeza umakini katika malezi ya watoto ili kuandaa watoto walio na tabia njema.
Taarifa Imetolewa na kitengo cha habari na uhusiano Jimboni Temeke