Home » » Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP)

Written By CCMdijitali on Wednesday, October 5, 2022 | October 05, 2022

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP) Mgeni Jailani Jecha, Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar Valentina Andrew Katema na Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar Shaheen Fauz Mohamed.
 
Hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa, Vyombo vya ulinzi na usalama na Viongozi wa dini.
 
Akizungumza baada ya uapisho huo Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Mgeni Jailani Jecha amesema kipaumbele chake katika utendaji wa nafasi hiyo ni kuhakikisha kesi za jinai hususan kesi za udhalilishaji zinafanyiwa kazi.
 
Naye Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Valentina Andrew Katema amesema atahakikisha anakwenda kusimamia misingi ya sheria na kanuni ambazo ndizo zinazomuongoza kwenye utendaji wa majukumu yake.
 
Naye Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar Shaheen Fauz Mohamed amesema atahakikisha anazisimamia fedha katika misingi ya haki na uadilifu.
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link