Haya yamesemwa na Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Hassan Surumbu wakati wa ziara yake ya kawaida kukagua maendeo yanayozunguka chanzo cha maji katika Kata hiyo tarehe 06.11.2022
Mkuu wa Wilaya amewapongeza Wananchi wa Kata hiyo kwa jitihada wanazozifanya katika kukabiliana na changamoto ya ukame kwa kuendelea kutunza chanzo hicho ambacho kimekuwa ni msaada mkubwa sana hasa kwao na maeneo jirani ikiwemo Kata ya Maramba ambayo ina idadi kubwa ya Wananchi.
Aidha Mkuu wa Wilaya amemuagiza Mwenyekiti kijiji kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa kitongoji kuhakikisha wananchi ambao bado wanaendeleza kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo yaliyoko pembezoni mwa chanzo kuhakikisha wanaacha mara moja kufanya shughuli hizo.
Pia amewaagiza Viongozi wa Kata hiyo kwa kushirikiana na Afisa Mazingira wa Halmashauri kuhakikisha Wanawasiliana na wamiliki wa migodi ambao walikua wanajihusisha na shughuli za uchimbaji apo awali kufukia mashimo waliyoyaacha wazi ikiwemo na kupanda miti kama walivyoagizwa.