Ukiachana na hotuba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini iliyoangazia masuala ya ushirikiano wa kimataifa, ukuzaji biashara na uwekezaji, utatuzi wa pamoja wa changamoto za kidunia na maboresho ya Umoja wa Mataifa.
Tanzania tumevuna vingi sana katika mkutano huu wa BRICS endapo tutajiunga na muungano huu tutakuwa katika kundi la nchi nufaika.
Kwa tathimini BRICS+ asilimia 45 ya mafuta yanayozalishwa Duniani au zaidi ya pipa milioni 37 zinazozalishwa kwa siku zinatoka katika Jumuiya hii.
Asilimia 50 reserve ya Gesi asilia inapatikana katika muunganiko huu wa nchi za BRICS+
Asilimia 30 ya GDP Dunia inapatikana katika nchi zinazounda muunganiko wa BRICS+
Kwa siku ya Jana Rais Samia alifanya mikutano midogo kando na mkutano wa BRIC+ jambo ambalo liliwavuta viongozi wengi zaidi kutaka kufanya vikao naye pamoja na kutafuta fursa za ushirikiano;
Kwa siku ya Jana pekee Rais Samia alifanya vikao takribani 9 na viongozi mashuhuri wa Dunia.
1. Mazungumzo na Rais wa China Xi jinping kikao cha pamoja.
2. Alikutana na Rais wa Brazil Lula Da Silva na kufanya naye kikao.
3. Alikutana na Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa na kufanya naye kikao
4. Alifanya mazungumzo na Rais wa Iran Seyyed Ibrahim Rais. Kikao cha kando
5. Alifanya kikao na Waziri Mkuu wa Bangladeshi Sheikh Hassina Wazeed.
6. Alifanya kikao na Rais wa Malawi Lazarus Chakwera
7. Alifanya kikao na Rais wa Senegal Macky Sall. Pamoja na kukutana na viongozi wengine mashuhuri yote ni katika kukuza diplomasia ya ushirikiano na kutafuta masoko ya pamoja.
Tunaweza kusema Rais Samia she is always step ahead katika kutazama fursa na kupanga mipango ya mbeleni.
#Mamayukokazini