Home » » DKT BITEKO AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA UBUNIFU NA MAFUNZO YA TAAARIFA ZA KIJIOGRAFIA

DKT BITEKO AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA UBUNIFU NA MAFUNZO YA TAAARIFA ZA KIJIOGRAFIA

Written By CCMdijitali on Saturday, September 9, 2023 | September 09, 2023

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko akikata utepe kuzindua kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya Taarifa za Kijiografia kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa tarehe 9 Septemba 2023.



 

Na Munir Shemweta, WANMM

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko amezindua kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya taarifa za kijiografia na kuitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kujitathmini katika utekelezaji majukumu yake ya msingi badala ya kuwa wizara ya inayoshughulika na utatuzi wa migogoro.

 

Dkt Biteko amesema hayo tarehe 9 Septemba, 2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya taarifa za kijiografia kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa.

 

“Kazi kubwa ya Wizara hii ni kupanga, kupima na kumilikisha ardhi, sasa tujipime na tujitathmini kama katika sekta yetu ya ardhi kazi hizi tunazifanya kwa ukamilifu wake’’ alisema.

 

Aidha, ameitaka Wizara hiyo kushirikiana na Halmashauri zote nchini ili kazi zifanyike kwa ushirikiano na kuondoa urasimu pamoja na migogoro ya ardhi.

 

Akigeukia kituo alichokizindua, Naibu Waziri huyo Mkuu na Waziri wa Nishati alisema, kituo hicho muendelezo wa hatua zinazochukuliwa na Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuchochea matumizi ya teknolojia sambamba na kuhakikisha ardhi inapangwa, inapimwa na kumilikishwa.

 

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa alisema, kituo kilichozinduliwa mbali na kusaidia kutoa ujuzi kwa watumishi kitawezesha pia kupunguza gharama sambamba na upimaji eneo kubwa kwa muda mfupi.

 

Alikielezea kituo hicho kuwa, ni muhimu kwa kuwa pamoja na mambo mengine kitaboresha shughuli za upimaji ardhi, uandaaji ramani za msingi, ujenzi wa miundombinu na kupanga matumizi bora ardhi.

 

Hafla ya uzinduzi wa kituo hicho ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.

 

 

--------------------------------MWISHO-----------------------------

 

 

         

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko (wa pili kulia), Waziri wa Ardhi Jerry Silaa (wa kwanza kulia) na Balozi wa Korea Mhe. Kim, Sun Pyo (wa pili kushoto) wakipiga makofi baada ya uzinduzi Kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya Taarifa za Kijiografia tarehe 9 Septemba 2023.

                   
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko (wa kwanza kulia) akipata taarifa za vifaa vya upimaji wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya Taarifa za Kijiografia tarehe 9 Septemba 2023.

                                                    

 


 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko akikabidhiwa ndege isiyotumia rubani na Balozi wa Korea Mhe. Kim, Sun Pyo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya Taarifa za Kijiografia tarehe 9 Septemba 2023.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko akimkabidhi ndege isiyotumia rubani Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya Taarifa za Kijiografia tarehe 9 Septemba 2023.


 


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya taarifa za Kijiografia tarehe 9 Septemba 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

 

 



Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link