Home » » TANZANIA KUSHIRIKIANA NA MOROCCO KATIKA MICHEZO

TANZANIA KUSHIRIKIANA NA MOROCCO KATIKA MICHEZO

Written By CCMdijitali on Wednesday, September 13, 2023 | September 13, 2023

 Na Eleuteri Mangi

 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Morocco hapa nchini Mhe. Zakaria El Goumiri kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Morocco katika Sekta ya Michezo.
 
Kikao hicho kimefanyika Septemba 13, 2023 katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salam ambapo Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro amewasilisha salamu za pole kwa nchi hiyo kufuatia Tetemeko la Ardhi lililopita katika nchi hiyo. Na kumhakikisha Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.  
 
 
Kwa upande wake Balozi Mhe. Zakaria El Goumiri amepokea salamu za pole kutoka Tanzania, ambapo pia amesema nchi yake itaiunga mkono Tanzania katika ujenzi wa miondombinu ya michezo ili kuendelea kukuza vipaji vya wanamichezo ambao watakuwa ni hazina kwa mataifa hayo kwenye timu za taifa.
 
Kikao hicho kimehudhuriwa pia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw.Saidi Yakubu ambaye amesema ushirikiano wa Tanzania na Morocco katika sekta ya michezo ni wa kihistoria na kila mara nchi hizo mbili zimekuwa na mechi za kirafiki katika nyakati tofauti na hivi karibuni timu moja kutoka nchi hiyo itakuja nchini kucheza na timu mojawapo.






Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link