Home » » AL HAJJ DK. HUSSEIN ALI MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA KIISLAMU KWENYE IBADA YA SALA YA IJUMAA.

AL HAJJ DK. HUSSEIN ALI MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA KIISLAMU KWENYE IBADA YA SALA YA IJUMAA.

Written By CCMdijitali on Friday, October 27, 2023 | October 27, 2023

RAIS WA ZANZIBAR AL HAJJ DK. HUSSEIN ALI MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA KIISLAMU KWENYE IBADA YA SALA YA IJUMAA.



Zanzibar,

27 Oktoba, 2023




RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa Kiislamu kwenye Ibada ya Sala ya Ijumaa, viwanja vya  Markas Bungi, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. 

Alhaj Dk. Mwinyi aliendelea kuikumbusha jamii juu ya kuamrishana mema na kukatazana maovu ili kuendelea kupata radhi za Mwenyezi Mungu (S.W) na taifa lenye maadili na kumcha Mungu.

Alisema, viongozi wa dini wananafasi kubwa kwa jamii kuwaelekeza mambo ya heri ili kupata jamii yenye busara, upendo, amani, umoja na mshikamano na kuongeza kuwa kupitia utengamano huo hata Serikali inapata fursa nzuri ya kuwaletea maendelo ya watu wake kwa ufanisi wa hali ya juu.

Alhaj Dk. Mwinyi aliwaeleza waumini hao kwamba, bado jamii inahitaji msaada mkubwa wa viongozi wa dini ili kurekebisha mitazamo ya waovu wachache, kwa kuyakataza na kuyakemea maovu yanayotendeka kupitia kundi la vijana ambao ni waathirika wakubwa kwenye suala la mporomoko wa maadili.

Alisema, viongozi hao wanamchango mkubwa kwa Serikali hususani kwenye suala zima la kujenga maadili ya umoja wa watu, suala ambalo linaleta mazingira mazuri ya maendeleo.

Sambamba na kuwaomba viongozi wa dini na waumini hao kuendelea kuliombea dua taifa na viongozi wake kupitia kazi kubwa wanayoifanya ya kulitumikia taifa.

“Sisi viongozi tunahitaji dua zenu kuombewa ili kutimiza majukumu yetu kwa ufanisi mkubwa” Alisisitiza Alhaj Dk. Mwinyi. 

Naye, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume, alipongeza juhudi za masheikh wa tablikh kwa kufanikisha majukumu yao kwa uadilifu mkubwa bila kuchanganya siasa na mikinzano isiyofaa kwa jamii, pia aliwaomba mashekh hao kuendelea kuwaombea Rais  Alhaj Dk. Mwinyi na viongozi wa nchi kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kulitumikia taifa. 

Akizungumzia umuhimu wa darsa za kufundishana mambo mema ya heri, Khatib wa sala ya Ijumaa viwanjani hapo Sheikh, Abubakar Mubarak, aliwaeleza waumini kwenye mkusanyiko huo na jamii kwa ujumla kwamba darsa za kiislamu hukusanya waumini wa chache kwenye eneo moja lakini kwenye mkusanyiko mkubwa kama huo uliokusanya miji, nchi na makabila tofauti yasiyojuana kukaa pamoja na kumtaja Allah (S.W) hupatikana zaidi radhi za Mwenyezi Mungu.









IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR.



Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link