DK.MWINYI KUFUNGUA KIKAO CHA 77 CHA KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA ARUSHA
Written By CCMdijitali on Friday, October 20, 2023 | October 20, 2023
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili Jijini Arusha kesho tarehe 20 Oktoba 2023 kufungua kikao cha 77 cha Kamisheni ya Umoja wa Afrika kinachohusu haki za binadamu na watu atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC.
Katika uwanja wa ndege wa Arusha amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella , Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Pindi Chana, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba , Sheria , Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman pamoja na viongozi mbalimbali wengine wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha na vyombo vya ulinzi na usalama.
🗓️19 Oktoba, 2023
📍Arusha.
Labels:
KITAIFA