Home » » MHE UMMY AGAWA MAJIKO NA MITUNGI YA GESI KWA MAMALISHE 315 JIJINI TANGA.

MHE UMMY AGAWA MAJIKO NA MITUNGI YA GESI KWA MAMALISHE 315 JIJINI TANGA.

Written By CCMdijitali on Monday, October 16, 2023 | October 16, 2023

Published from Blogger Prime Android App
#OdoUmmyJimboni #mchetuwakazi 
------


Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Ummy  Mwalimu leo tarehe 15/10/2023 amegawa majiko ya gesi 80 mitungi mikubwa ya gesi (ya kilo 15) 80 na meza 80 na kreti za soda 80 kwa wajasiliamali wanawake wanaojihusisha na biashara ya Chakula (Mama Lishe/Mama Ntilie) wa Jijini Tanga. Ambapo jumla ya wanawake wajasiriamali 315 watanufaika na vifaa hivi.

Vifaa vilivyotolewa chini ya Kampeni ya Mwanamke Shujaa vimedhaminiwa na  Kampuni ya Cocacola Kwanza na Oryx Gas Tanzania kupitia Kampeni yenye Kauli mbiu ya "Mwanamke Shujaa" Jiamini, Jithamini na Jijenge". Kampeni hii pia imewashirikisha Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Korogwe FM na TK FM Radio ya Tanga.

Aidha Mhe Ummy amewachangia katoni  za soda 160 ambapo kila biashara ya Mama Lishe itapata katoni 2.

Mhe Ummy amewashukuru CocaCola na Oryx kwa kuunga mkono jitihada zake Mbunge wa Tanga Mjini na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kuwawezesha wanawake kiuchumi. Aidha Mhe Ummy amewashukuru kwa kukubali ombi lake la kuja Tanga awamu ya pili ili kuwapatia Mama Lishe vifaa hivi muhimu vya mtaji ili kuwawezesha kiuchumi. 

Akiongea katika ghafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Cocacola bwans Unguu Sulay ameeleza kuwa Kampuni ya CocaCola itaendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia kwa kuwezesha wananchi kiuchumi hususani wanawake.  Aidha ameeleza kuvutiwa na kazi kubwa na nzuri ya Mhe Ummy katika kuwatumikia watanzania na wananchi wa Tanga Mjini na ndio maana wameamua kumuunga mkono.

Hafla hiyo ya kukabidhi mitungi, majiko ya gesi na meza na kreti moja yenye soda, imehudhuriwa na Naibu Meya wa Jiji la Tanga Mhe Rehema Mhina, Mkurugenzi Mkuu wa CocaCola ndugu Unguu Sulay,  ndugu Kaimu Mkurugenzi Jiji la Tanga Kizito na viongozi wa CCM na wajasiriamali wanawake wa Tanga Mjini.

Imetolewa na;
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Tanga Mjini
15/10/2023.










Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link