Home » » "NITAHAKIKISHA KITUO CHA AFYA, BARABARA MLIMA LYAMBA LYA MFIPA KUJENGWA" CHONGOLO

"NITAHAKIKISHA KITUO CHA AFYA, BARABARA MLIMA LYAMBA LYA MFIPA KUJENGWA" CHONGOLO

Written By CCMdijitali on Thursday, October 12, 2023 | October 12, 2023

 




Katibu Mkuu wa CCM Komredi Daniel Chongolo akitoa Saini kwenye kitabu Cha wageni aliposhiriki katika kikao cha shina namba 9 Tawi la Kalakala, Kata ya Muze, Sumbawanga Vijijini Oktoba 10, 2023, wakati ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama ya 2020-2025.





Chongolo, ameahidi kwenda kusukuma serikali kupeleka haraka fedha za ujenzi wa Kituo Cha Afya na kuhakikisha ujenzi wa barabara inayopita Mlima Lyamba lya mfipa inayokwenda katika kata ya Muze Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga unaharakishwa.



Komredi Chongolo akiwa na Mwenyekiti wa Shina hilo, Salvatore Kasima.


Sehemu ya wanachama na wapenzi wa CCM pamoja na wajumbe wa Shina hilo wakiwa katika kikao hicho.


Mwenyekiti wa Shina Kasima akifungua kikao hicho.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere akijitambulisha kwa wananchi. Kushoto ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile.


Katibu wa NEC Oganaizesheni CCM,  Issa Haji Gavu akihutubia katika kikao hicho.Amewaahidi wanachama wa CCM wa eneo kuanza kupata kadi moya za kielektriniki.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
 

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link