Home » » RC MONGELLA AWAAGIZA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUBUNI VYANZO ENDELEVU VYA MAPATO

RC MONGELLA AWAAGIZA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUBUNI VYANZO ENDELEVU VYA MAPATO

Written By CCMdijitali on Monday, October 16, 2023 | October 16, 2023



Na Elinipa Lupembe

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa huo, kubuni vyanzo endelevu vya mapato ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuziwesha halmashauri hizo kujiendesha bila mikwamo.

Mhe. Mongella amewahimiza viongozi hao kuachana na vyanzo ambavyo havidumu na kufikiria namna ya kuwa na vyanzo ambavyo havifi, vyanzo ambavyo vitaziwezesha halmashauri hizo kujitegemea katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazotegemea Mapato ya Ndani.

"Mnapaswa kuacha kutegemea vyanzo vya kuuza viwanja, ambavyo hupandisha makusanyo na pindi vinapokwisha mapato yanashuka, ushuru wa mazao sio vyanzo vya kuvitegemea havina uhakika pia, vinategemea mvua, hali ya hewa ikibadilika mapato yanayumba, jipangeni kutafuta vyanzo endelevu na sio hivyo vya kupita" Amesisitiza Mhe. Mongella.

Aidha amewatahadharisha  kuhakikisha usimamizi thabiti wa fedha za miradi inayoletwa kutoka serikali kuu, kwa kuzingatia maelekezo yake na  kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa fedha zilizoletwa na sio kuongeza fedha kutoka mapato ya ndani.

"Serikali inaleta fedha za miradi zikiwa na maelekezo kamili ya kukamilisha mradi, haiwezekani wengine wakamilishe na wengine waseme fedha hazitoshi, kila mkurugenzi ahakikishe anazinhatia ameleekzo ya fedha za serikali na si vinginevyo.

Aidha amekea tabia ya baadhi ya halmashauri kuchelewa kukamilisha miradi kwa kuwa serikali inatoa fedha za miradi zikiwa kamili na maelekezo ya utekelezaji, hivyo ni vema kila mkurugenzi na watalamu wakazingatia maelekezo ya utekezaji wa miradi inayoletewa fedha kutoka serikali kuu.

Awali mkuu huyo wa mkoa amekutana na Watalamu wa Idara za Fedha na Ukaguzi wa Ndani kutoka halmashauri saba za mkoa wa Arusha, wakati wa kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa mkoa Arusha.

Kikao kazi hicho chenye lengo la kujadili masuala ya Hoja za Ukaguzi,  mapato na matumizi pamoja na usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya halmashauri.








#arushafursalukuki
#kaziinaendelea
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link