Na Eleuteri Mangi, WUSM
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Bw. Richard Mganga amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli za chuo hicho ambacho ni ni chuo pekee kinachotoa mafunzo ya michezo kwa wataalamu wa michezo nchini.
Chuo hicho kipo mkoani Mwanza katika Wilaya ya Kwimba ambapo jukumu lake kuu ni kufundisha taaluma ya michezo, kutafiti na kutoa ushauri kuhusu masuala ya maendeleo ya michezo.
Ili kufikia azma hiyo ya Serikali, Bw. Maganga amesema chuo hicho kinaendelea na ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuchukua wanachuo takriban 192 kwa wakati mmoja ili kuongeza idadi ya wataalam wa michezo nchini.
Bw. Mganga amesema hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuchukua wastani wa wanachuo 48 kwa kila ghorofa na itakuwa na vyumba nane vya kusomea, vyoo pamoja na sehemu ya kufulia na kunyoshea nguo.
Mradi huo wa ujenzi wa hosteli ya Ghorofa tatu linatarajiwa kutumika kwa ajili ya makazi ya wanafunzi na upo chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo unakadiriwa kutumia kiasi cha Shilingi 2,562,032,000 hadi kukamilika kwake ambapo hadi sasa Wizara imepokea kiasi cha Tshs 1,699,156,86.
Ujenzi wa hosteli hiyo umefikia asilimia 69 ikukamilika mwakani 2024 itasaidia kuongeza ya idadi ya wanafunzi chuoni hapo kwa kuwa hosteli inayotumika sasa inauwezo wa kuchukua wanafunzi 128.
Home »
MICHEZO NA BURUDANI
» UJENZI WA HOSTELI MALYA KUONGEZA UDAHILI WA WANACHUO
UJENZI WA HOSTELI MALYA KUONGEZA UDAHILI WA WANACHUO
Written By CCMdijitali on Sunday, October 8, 2023 | October 08, 2023
Related Articles
- WAZIRI UMMY ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA UTAMBUZI NA ELIMU JUU YA SARATANI.
- TANZANIA YAPOKEA OMBI LA PALESTINA KUANZISHA KITUO CHA MICHEZO
- TANZANIA KUWASILISHA OMBI CAF MATUMIZI YA MATANGAZO YA KISWAHILI
- WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASISITIZA KUWATUMIA WACHEZAJI WENYE ASILI YA TANZANIA WALIO NJE YA NCHI, AAGIZA WIZARA HUSIKA ZIKUTANE
- DKT. NDUMBARO AIAGIZA MIKOA KUJIANDAA VYEMA MASHINDANO YA SAMIA TAIFA CUP
- MAKAMPUNI JITOKEZENI KUFADHILI VILABU VYA SOKA NCHINI
Labels:
MICHEZO NA BURUDANI
Post a Comment