Home » » RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA DK.JUAN PABLO

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA DK.JUAN PABLO

Written By CCMdijitali on Monday, November 6, 2023 | November 06, 2023

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Dunia anayeshughulikia masuala ya Afya Dk.Juan Pablo na ujumbe wake Ikulu Zanzibar


Zanzibar,


06 Novemba, 2023

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameshukuru ushirikiano wa karibu uliopo baina ya Tanzania hususani Zanzibar, na Benki ya Dunia (WB), Umoja wa Ulaya (EU) na ushirikiano wa diplomasia uliopo baina ya Australia na Tanzania.

Dk. Mwinyi alitoa shukurani hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na wageni hao walioambatana na ujumbe waliofuatana nao kwa nyakati tofauti.
Alisema, taasisi hizo zinamchango mkubwa wa maendeleo ya Zanzibar hasa kukuza sekta ya Afya nchini, Elimu, Utalii na Uchumi wa Buluu.

Akizungumza na Balozi wa Australia nchini Tanzania, Mhe. Luke William aliefika kumuaga, Rais Dk. Mwinyi alishukuru ushirikino mkubwa uliopo baina ya Tanzanzia na nchi hiyo na kumueleza juu ya Zanzibar inavyonufaika na sekta ya uvuvi na mwani uliowaneemesha kinamama wengi na vijana kwani asilimia 90 ya wakulima wake ni kina mama.

Pia, Rais Dk. Mwinyi alimueleza balozi huyo azma ya kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Austalia na Zanzibar hasa kwenye masuala ya uwekezaji, biashara na utalii.

Vile vile Rais Dk. Mwinyi alizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya Bahari na Uvuvi wa Umoja wa Ulaya (EU), Bi. Charlina Vitcheva alimueleza kuwa Zanzibar ni kisiwa kilichozungukwa na bahari ya Hindi, kinajivunia fursa nyingi zinazotokana na rasilimali bahari kwa kujikita zaidi kwenye uchumi wa Buluu na Utalii.

Alimueleza Mkurugenzi  huyo, Uchumii wa Buluu ni sekta muhimu kwa uchumi wa Zanzibar na kuongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inafanya kila iwezavyo kunufaika na fursa zinazotokana na sekta hiyo kwa ajili ya uchumi na watu wake.

Aidha, alimueleza mgeni huyo kuimarisha zaidi ushirikiano wao kwenye sekta hiyo, ili kujenga uweledi kwani idadi kubwa ya Wazanzibari wamejikita zaidi na masuala ya uvuvi na ajira zinazotona na bahari.

Rais Dk. Mwinyi alisema, Serikali pia inawaungamkono wavuvi na wakulima wa mwani nchini kwani imewawezesha kwa mitaji na vifaa pamoja na kuiungamkono sekta ya Utalii.

Kwa upande wao wageni hao walemueleza Rais Dk. Mwinyi juu ya kuendelea kuiungamkono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla hasa kwenye masuala ya kuendeleza ushirikiano wao wa diplomasia na kuona fusra za uwekezaji na uchumi zilizomo Tanzanzia vinanufaisha pande zote na ushirikiano wao.









IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link