Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella akifungua Mkutano Mkuu wa 6 mwaka 2023 wa Chama cha Watalam wa Udhibiti wa Ufisadi, Rushwa na Ubadhilifu (ACFE) Tanzania, unaofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Hoteli ya Mount Meru Hoteli jijini Arusha.
Mhe.Mongella amefungua mkutano huo wa siku tano, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Haroon Ali Suleiman.
Mhe. Mongella ametumia fusa hiyo kuwapongeza Waheshimiwa Marais, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa jitihada na nia thabiti wanayoionesha kwa vitendo katika kupambana na Rushwa, Ubadhirifu pamoja na Ufisadi ambavyo vimekua sumu kubwa inayorudisha nyuma maendeleo.
Aidha Mada ya kuvutia kwa mkutano wa mwaka huu ni "MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA NA UBADHIRIFU KATIKA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO NA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIJAMII"
@rc_mkoa_arusha @acfetanzania @acfeindonesia.chapter111 @wizaramnn #ccmdijitaliupdates