SERIKALI KUENDELEA KUWABEBA WATUMISHI WANAOFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU-KIKWETE.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete aliyasema hayo Bungeni wakati Swali ya Mbunge wa Same Mashariki Ndg. Anna Kilango Malecela .
Naibu Waziri alisema, Serikali imeendelea kutoa motisha ya kifedha na isiyo ya kifedha kwa watumishi wote ikiwemo watumishi wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu kwa kuboresha viwango vya posho ya kazi baada ya masaa ya kazi, posho ya kujikimu wakati wa kusafiri, posho ya mawasiliano, kufikisha huduma ya umeme katika maeneo yao, kutoa magodoro, kutoa nyumba za walimu zenye staha na mengine mengi.
Akijibu swali la Ziada, alimuhakikishia Mbunge na Bunge kuwa Serikali inatambua changamoto za Watumishi katika Halmashauri yao na nyengine Nchini kwa kuwa iko timu iliyokwisha zunguka nchi nzima kukagua mazingira ya Watumishi hivyo upatikanaji wa fedha na mipango ya huduma kwa Watumishi itawahakikishia mazingira mazuri ya Watumishi wanaofanya kazi katika mazingira Magumu.
#KaziInaendelea #Bungeni