MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA MKUTANO WA BODI YA GPE MJINI UNGUJA LEO
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah leo amefungua rasmi mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ushirika wa Maendeleo ya Elimu Duniani (GPE) unaoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hio, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, hoteli ya Zanzibar Hyatt, Unguja, leo.
Mkutano huo wa siku mbili, unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na nje ya Marekani na Ulaya, tangu Shirika hilo lianzishwe na mataifa tajiri duniani ya G7 miaka 20 iliyopita.
Kwa mujibu wa Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza GPE, shirika hilo hadi sasa limeishaipatia Tanzania jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu Tanzania bara na Zanzibar.
Bodi ya Wakurugenzi ya GPE inaundwa na majimbo 20 yanayowakilisha washirika wote wa ushirikiano, ambapo katika mkutano wa bodi wanahudhuria Mjumbe wa Bodi na mjumbe mbadala wa Bodi wanawakilisha kila jimbo.
Bodi ya Wakurugenzi ya GPE huweka sera na mikakati ya ushirikiano, huku ikiakisi hali pana na tofauti ya ubia na inajumuisha wanachama kutoka serikali za nchi zenye mapato ya chini na washirika wote wa maendeleo: wakiwemo wafadhili, mashirika ya kiraia, sekta binafsi na wakfu, na mashirika ya kimataifa na benki za kikanda.
Nchi washirika wa GPE ni Afghanistan, Albania, Algeria, Angola, Bangladesh, Belize, Benin, Bhutan, Bolivia, Burkina Faso, Burundi, Cabo Verde, Cambodia, Cameroon, Central African Republic, Chad, Comoros, Congo, Democratic Republic ofCongo, Republic of, Côte d'Ivoire, Djibouti, Dominica, na Egypt.
Nchi zingine ni El Salvador, Eritrea, Eswatini, Ethiopia, Fiji, The Gambia, Georgia, Ghana, Grenada, Guatemala, Guinea, Guinea-Bissau, Guyana, Haiti, Honduras, India, Indonesia, Kenya, Kiribati, Kyrgyz Republic, Lao PDR, Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Maldives, Mali, Marshall Islands, Mauritania, FS Micronesia, Moldova, Mongolia na Morocco.
Zingine ni Mozambique, Myanmar, Nepal, Nicaragua, Niger, Nigeria, Pacific region, Pakistan, Papua New Guinea, Philippines, Rwanda, Saint Lucia, Saint Vincent and the Grenadines, Samoa, São Tomé and Príncipe, Senegal, Sierra Leone, Solomon Islands, Somalia, South Sudan, Sri Lanka, Sudan, Tajikistan.
Tanzania, Timor-Leste, Togo, Tonga, Tunisia, Tuvalu, Uganda, Ukraine, Uzbekistan, Vanuatu, Viet Nam, West Bank and Gaza, Yemen, Zambia na Zimbabwe pia ni nchi washirika. Syria si nchi mwanachama lakini imepokea ufadhili kwa idhini ya Bodi ya GPE.