Home » » RC KINDAMBA AWAASA TANGA KUSHIRIKI UWEKEZAJI WA NDANI

RC KINDAMBA AWAASA TANGA KUSHIRIKI UWEKEZAJI WA NDANI

Written By CCMdijitali on Friday, January 19, 2024 | January 19, 2024

Published from Blogger Prime Android App

Na Zuberi Mgaya , MUM-TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Waziri Kindamba amewataka wakazi wa mkoa huo kutumia fursa za ki-uchumi kushiriki katika uwekezaji wa ndani ili kukuza uchumi wao na taifa.

Mhe Kindamba ameyasema hayo leo, Januari 19, 2024 ofisini kwake alipozungumza na ujumbe kutoka Kituo cha Uwekezaji (TIC) unaohamasisha mabadiliko ya fikra kuhusu uwekezaji na wazawa kushiriki uwekezaji wa ndani. 

Mhe Kindamba amesema hali ya uchumi wa mkoa na wakazi wa Tanga inazidi kuboreka, akitolea mfano ukuaji wa pato la taifa (GDP) mkoani humo kutoka Shilingi Shilingi Trilioni 5.7 kwa mwaka 2018 kufikia Trilioni 7.9 kwa mwaka 2022 na kipato cha mtu mmoja mmoja kutoka Shilingi milioni 2.4 (2018) kufikia Shilingi milioni 3  kwa mwaka 2022.

Mhe Kindamba amesema, Serikali imejidhatiti kuimarisha, kuongeza na kuendeleza viwanda na biashara, na kutoa kipaumbele kwa biashara ya mazao ya mkonge, korosho na mihogo.

Amesema jitihada hizo zimefanikisha kupatikana wawekezaji kwenye viwanda vya kuchakata muhogo wilayani Handeni kitakachogharimu Dola za Marekani milioni 50 na kile cha samaki ambacho mchakato wa uwekezaji wake unaendelea.

Miongoni mwa sekta alizozitaja kuwa sehemu ya fursa za uwekezaji ni utalii hususani kwenye fukwe za bahari, ukanda wa milima ya Lushoto na misitu ya asili iliyopo wilayani Muheza.


Mhe Kindamba amezielekeza mamlaka za udhibiti mkoani humo, zijiepushe na hulka ya kufunga biashara za wawekezaji wenye kasoro, badala yake wafanye mazungumzo na kutoa elimu ya namna bora ya kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza sekta hiyo.

Awali Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Pili Mnyema, amesema mkoa huo umeweka mikakati ya kuwawezesha wananchi wake kuzing’amua na kuzitumia fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani humo.

Naye Meneja wa Uhamasishaji na Uwekezaji wa Ndani wa TIC, Ndugu Felix John, amewataka wanachi kubadili fikra na mitazamo yao kutoka katika kuamini kwamba ni uwekezaji unawahusu raia wa kigeni peke yao.


Mwandishi wa Habari hii ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya Mawasiliano kwa Umma katika Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM).

Mwisho.

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link