Home » » SERIKALI YAENDELEA KUSHUSHA GHARAMA ZA ULETAJI MAFUTA KULETA AHUENI KWA WANANCHI

SERIKALI YAENDELEA KUSHUSHA GHARAMA ZA ULETAJI MAFUTA KULETA AHUENI KWA WANANCHI

Written By CCMdijitali on Friday, January 19, 2024 | January 19, 2024

Published from Blogger Prime Android App

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, juhudi zinazofanywa na Wizara ya Nishati, Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) zimepelekea gharama za uletaji wa mafuta nchini (premium) kuendelea kushuka na hivyo kuchangia katika unafuu wa gharama za mafuta ikiwemo ya dizeli na petroli. 

Amesema hayo tarehe 19 Januari 2024 jijini Dodoma wakati Wizara ya Nishati ilipowasilisha taarifa kuhusu mwenendo wa biashara ya mafuta  nchini kwa kipindi cha mwezi Septemba hadi  Disemba 2023, kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. Kikao ambacho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, Katibu Mkuu, Mhandisi, Felchesmi Mramba, baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Watendaji wa Wizara ya Nishati. 

“ Wizara ya Nishati, EWURA na PBPA, kwa kweli wamefanya kazi kubwa mno ya kushusha gharama za uagizaji mafuta kutoka nje ya nchi, hapo awali gharama hizi zilikuwa zikiongezeka kila mwezi lakini wamesimamia vizuri suala hili na gharama hizi zimeanza kushuka na hivi karibuni mlisikia Waziri wa Kenya akisema bei za mafuta nchini humo zipo juu na za Tanzania zipo chini sababu ya premium, na wengine pia walio nje wanatoa ushuhuda kwamba walau sisi gharama zetu zina unafuu.” Amesema Dkt. Biteko 

Dkt. Biteko ameeleza kuwa PBPA ambayo inasimamia uagizaji wa mafuta kwa pamoja, ina umuhimu mkubwa nchini kwani ndiyo inayopelekea nchi kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta yanayotosheleza mahitaji ya nchi na yenye viwango vya ubora unaohitajika,  Serikali kufahamu kiwango cha mafuta kinachoingia nchini, kupanga ukusanyaji wa mapato kwa kutumia takwimu sahihi na kupanga bei elekezi ya mafuta.

Amesema kuwa, Serikali itaendelea kuisimamia kwa ukamilifu Taasisi hiyo ili iendelee kufanya kazi kwa ufanisi kwani tayari imekuwa ni mfano wa kuigwa kwa nchi zinazotuzunguka na kuwataka watendaji wa Taasisi hiyo kufanya kazi kwa maadili na bila kumuonea mtu yeyote.

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link