Asema Rais Dkt. Samia ametoa shilingi bilioni 130 kwa ajili ya ukarabati madaraja mkoa wa Lindi. Awatoa hofu wakazi na watumiaji wa barabara ya Dar, Lindi. WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amet ...

Read more »

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ikiwemo kuimarisha hali ya u ...

Read more »

 Na Mwandishi wetu, ArushaMamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imeendelea na zoezi la kuwajengea uwezo wazabuni kuhusu matumizi ya Moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufa ...

Read more »

 Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Vivin Method akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati akifungua Mafunzo kuhusu Upimaji wa Afya yaliyofanyika jijini Dar es Sa ...

Read more »

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Ukraine zimekubaliana kuongeza ushirikiano katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii ikiwemo kilimo, biashara na uwekezaji, viwanda, utalii, elimu n ...

Read more »

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amewasili jijini Antalya, Uturiki kwa ziara ya kikazi anayotarajia kuifanya nchini humo kuanzia Aprili ...

Read more »

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa Ziara yake Uingereza imekuwa na Manufaa Makubwa kwa Zanzibar kwani Wawekezaji wengi wameonesha dhamira ya k ...

Read more »

Na Mwandishi WetuMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Stephen Wasira amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo hakina hoja ya msingi ya kuzuia Uchaguzi Mkuu mwaka huu kwani kama ni mabadilik ...

Read more »

MAJALIWA AIPA MAAGIZO TANROADS UKARABATI WA BARABARA NA MADARAJA

Asema Rais Dkt. Samia ametoa shilingi bilioni 130 kwa ajili ya ukarabati madaraja mkoa wa Lindi.   Awatoa hofu wakazi na watumiaji wa baraba...

Latest Post

NAIBU WAZIRI PINDA AELEKEZA UENDELEZAJI MIJI KUZINGATIA MIPANGO KABAMBE

Written By CCMdijitali on Tuesday, February 6, 2024 | February 06, 2024



Published from Blogger Prime Android App




Na Munir Shemweta, WANMM

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakikisha maendelezo yoyote yanayofanyika yanazingatia na kufuata mipango kabambe ya maeneo husika

Mhe. Pinda ametoa kauli hiyo tarehe 6 Februari 2024 Bungeni Dodoma wakati aikijibu swali la nyongeza la Mbunge wa jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula aliyetaka kujua ni nini mikakati ya serikali kuhakikisha maendelezo yanayofanyika kwenye halmashauri hayavunji au utekelezaji wake hauendi kinyume na mpango kabambe kwa kufanyiwa matumizi mengine yasiyokusudiwa.

Kwa mujibu wa Mhe. Pinda baadhi ya meneo hasa majiji makubwa tayari yana mipango mahususi (mpango kabambe) ya kuendelezwa ikiwemo jiji la mwanza lakini kumekuwa na utofauti katika kusimamia kile ambacho halmashauri imejipangia kwenye utekelezaji wa mipango kabambe ya miji yao.

‘’Nitoe rai kwa mamlaka za miji na majiji kuzingatia yaliyopitishwa na mamlaka zao kwa kuhakikisha miji inatoka na sura nzuri sana kwa kuzingatia mipango kabambe na hili la Mwanza wazingatie kile walichokubaliana’’. Alisema Mhe. Pinda

Akielezea zaidi kuhusiana na suala la jiji la Mwanza, Mhe. Pinda alitoa msisitizo kwa jiji hilo kuzingatia kile walichokubalina kwenye mpango kabambe kwa kuwa kiasi kikubwa cha fedha kimetumika wakati wa kuandaa mpango huo wa uendelezaji katika jiji hilo.

Awali Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Asia Sharif Omar alisema, kumekuwa na ujenzi holela katika maeneo mbalimbali licha ya uwepo sheria zinazoweka masharti ya ujenzi katika miji nchini.

Amebainisha kuwa, chanzo kikubwa cha ujenzi holela ni ukuaji wa kasi miji midogo kutoka vijiji unaotokana na shughuli za kibinadamu ambapo amesema kuwa, kutokana na hali hiyo wizara yake imekuja na mikakati ya kupima nchi nzima hadi vijijini.

Kwa mujibu wa Mhe. Pinda kampeni ya kupima vijiji inayofanywa na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi sambamba na upimaji miji unaofanywa na halmashauri kwa ushirikiano na wizara ni sehemu ya juhudi za kupambana na ujenzi holela.

Aidha, alisema ipo miradi ya urasimishaji wa makazi na upimaji shirikishaji aliyoieleza kuwa ni mikakati ya kupamabana na ujenzi holela  na kuweka wazi kuwa Serikali itaendelea kukabiliana na changamoto za ujenzi holela usiozingatia taratibu.

----------------------------MWISHO-------------------------------------                                                                                                               

PICHA YA MHE. GEOPHREY PINDA, NAIBU WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

 

1234567 Next

SPORTS

 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link