Home » » DKT. MPANGO AAGIZA KUKAMILIKA UJENZI WA BARABARA YA MALAGARASI -UVINZA IFIKAPO MACHI 2025.

DKT. MPANGO AAGIZA KUKAMILIKA UJENZI WA BARABARA YA MALAGARASI -UVINZA IFIKAPO MACHI 2025.

Written By CCMdijitali on Monday, July 8, 2024 | July 08, 2024


Published from Blogger Prime Android App

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kuhakikisha anasimamia ujenzi wa barabara ya Malagarasi - Ilunde - Uvinza (km 51.1) kwa kiwango cha lami ukamilike ifikapo mwezi Machi, 2025.

Dkt. Mpango ametoa agizo hilo leo Julai 8, 2024 katika eneo la Malagarasi wakati akikagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Malagarasi - Ilunde - Uvinza kwa kiwango cha lami na kuridhishwa na maendeleo yake.

“Hii barabara imesuasua sana hasa kipindi cha mvua, na huku Kigoma bado tunapata mvua nyingi kwa hiyo Waziri tutumie kipindi hiki cha kiangazi kukimbiza hii barabara iishe kama ulivyoahidi na sisi tupite hapa tukiwa tumevaa suti, Simamieni hili Waziri pamoja timu yako”, ameeleza Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango amesema kuwa wananchi wa Kigoma wameisubiria barabara ya Uvinza - Malagarasi kwa muda mrefu na ni muda sasa ikamilike na wananchi waweze kuendelea  kufanya biashara na kukuza uchumi wa Mkoa.

Amesisitiza kuwa uwepo wa miundombinu bora ya barabara kutaufanya Mkoa wa Kigoma kuwa Kitovu cha biashara na Mikoa mingine pamoja na nchi za jirani na kuwezesha wawekezaji kufika na kuwekeza katika Mkoa huo. 

Dkt. Mpango ameagiza Mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi na kuhakikisha hawapotezi ubora na viwango vilivyowekwa kwa mujibu wa Mkataba.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa kipindi cha nyuma mradi wa ujenzi wa barabara ya Uvinza - Malagarasi ulikuwa una suasua hivyo Wizara ilichukua hatua  ya kumuondoa Mhandisi Mshauri na kuleta Mhandisi Mshauri mwingine na sasa hivi ujenzi unaendelea vizuri.

Ameeleza kuwa baada ya hatua hiyo utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo hivi sasa unafanyika usiku na mchana na amemuahidi Makamu wa Rais kuisimamia barabara hiyo ikamilike kwa mujibu wa mkataba ifikapo mwezi Machi, 2025.


 @wizara_ya_ujenzi

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App

Published from Blogger Prime Android App
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link