Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miradi ya Wizara amekagua miradi ya maendeleo iliyoko jijini London, Uingereza kuanzia tarehe 14 hadi 18 Julai, 2024.
Katika ziara hiyo Kamati imekagua jengo la ofisi, makazi na kiwanja cha serikali. Vilevile, imefanya kikao cha mashauriano na ubalozi na wataalam wa ujenzi na uwekezaji nchini humo juu ya namna bora ya kuendeleza milki hizo za Serikali.
Katika ziara hiyo Kamati pia imekabidhi nyumba moja kwa mtumishi wa Ubalozi ambayo ukarabati wake umekamilika kwa asilimia 100 na hivyo kupunguza gharama za kulipia kodi ya pango kwa Serikali ambayo imekuwa ikilipwa kabla ya kukamilika kwake.
Ziara hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa mpango mahsusi wa Wizara wa kuendeleza viwanja na milki zake zilizopo nje ya nchi, ambao ulielezwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.) wakati alipowasilisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 bungeni jijini Dodoma mwezi Mei, 2024.
Ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ikiendelea. |
Picha ya pamoja. |